Nini husababisha kichaa cha mimba?

bushland

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2015
Posts
7,015
Reaction score
4,985
naomba kujua kuhusu hili tafadhali na pia naomba kujua ni njia gani itumike kuondoa tatizo hilo? nazungumzia kichaa cha mimba baada ya mwanamke kujifungua
 
naomba kujua kuhusu hili tafadhali na pia naomba kujua ni njia gani itumike kuondoa tatizo hilo? nazungumzia kichaa cha mimba baada ya mwanamke kujifungua

Kwanza pole kama umekutana na kadhia hii!

pili nipende kukujibu kuwa huu si uchawi wala ndumba ila bahati mbaya kinachosababisha Kichaa cha uzazi katika literature nyingi za kitabibu hakijawa documented japo indhaniwa kwamba wanawake wanaopata kichaa cha uzazi wanakua na viwango vichache vya hormone inaitwa Estradiol i.e Estradiol Deficiency

Inadhaniwa hiki ndo kisababishi maana ukiwapa wanawake hawa Hii hormone ya estradiol tatizo hili huwai kuisha kabisa.
Na viwango vya hormone hii vikipimwa kwa wanawake hawa huwa chini!

upimaji wa hormone hii kwa tanzania unapatikana kwa hospitali zote zinazoweza kufanya Hormonal profiles.
Ila sijajua upatikanaji wa hormone ya estradiol kwa Tanzania kama waweza kuonana na Obstetricians nafikiri watakusaidia maeneo ambako unaweza kupewa dawa hiyo

Kibongo bongo wanawake wengi wa hivi upewa dawa za wagonjwa wa akili ambazo lengo lake ni kumtuliza tu ila kiini halisi hakitibiwi.

Eneo hili bado linaitaji tafiti zaidi.
 
Kweli mdau!! Kuna mtumishi mwenzangu alifia mujmbili kabisa tatizo ni hilo. Yaani hakuna na shida yoyote ya kipesa wala mahusiano lkn alifariki. Niliumia na kuona huu mgonjwa hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…