Mr. MTUI
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 8,130
- 8,362
Habarini na heri ya Ijumaa kuu..
Napenda kuwapa stori hii...
Juzi nimekutana na rafiki yangu mwenye jinsia yakike niliyeachana naye kitambo sana tangu enzi za chuo....Tulikua kwenye basi moja tukitokea mkoani kwenye majukumu mbalimbali ya kujenga taifa hili la 'HAPA KAZI TU'...
Alikua ni mtu wa kujihisi na Ilinibidi nimshangae rafiki yangu huyo wa kike kwani alikua ameota ndevu nyingi sana kidevuni kiasi kwamba amekata tamaa ata ya kuzinyoa tena mfano wa huyo aliyepo pichani....
Katika pitapita zangu za kujielimisha nmeona nije na hii ili tuweze share ujuzi na idea mbalimbali hasa sababu za wadada kuota ndevu na vinyweleo kupita kiasi....
Kwa zamani watu walikua wakisema ukimuona mwanamke anandevu basi ujue ni tajiri....
WATAALAMU WANASEMAJE?
Kuota kwa nywele na vinyweleo vingi kwenye maeneo ambayo si yakawaida kwa mwanamke kitaalamu inaitwa Hirsutism. Mara nyingi nywele hizo zinaota maeneo ambayo tumezoea kuyaona kwa wanaume kama vile kifuani, tumboni, mgongoni, kidevuni, mustache n.k.
NINI KINASABABISHA UOTAJI HUU WA NYWELE?
Kunasababu nyingi zinazosababisha kuota kwa nywele kusipokuwa na mpangilio kwa wanawake sababu kuu ikiwa ni kuwepo kwa wingi kwa homoni ya kiume iitwayo ANDROGEN....Wanawake wote huwa wana homoni hii katika kiwango kidogo ukilinganisha na wanaume. Kuongezeka kwa kiwango cha hormon hii husababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo matumizi ya vipodozi na madawa.
- Baadhi ya madawa hasa yale ya kusisimua misuli kama yanayotumiwa na wanariadha husababisha kuongezeka kwa androgen kwenye damu...
- Mabadiliko ya hormon hasa wakati wa menopause nayo huweza sababisha uotaji wa ndevu au vinyweleo
- Matumizi ya vipodozi hasa vyenye steroid
- N.K