Titus pole sana
Tatizo hili hukumba watu wengi sana, Moja ya sababu kuu ni makuzi kuanzia nyumbani kama mtoto hajengewi mazingira ya kujiamini ni tatizo, eg mtoto anapotaka kusema kitu wazazi wakamcheka au kumwambia anyamaze basi mara nyingi atajenga hofu hata kuongea kwa wenzake.
Pia mashuleni, kama walimu hawawapi wanafunzi kujibu maswali, kujadiliana, kufanya debate basi watoto huwa na woga wa kuongea mbele za watu.
Jaribu hatua hizi chache
1. Jiandae ipasavyo kwa mada utakayoongelea-Pitia taratibu mada na ijue inside out
2. Fanya zoezi: baada ya kujiandaa basi fanya zoezi la kutoa mada hiyo ,mualike rafiki yako akusikilize na kukukosoa.Ukiwa fiti jiweke sawa kwa siku yenyewe kwa mavazi nadhifu.
3. Presentation;
a) Kupunguza hofu salimiana na audience wako wanapoingia chumba cha presentation
b) Anza kwa kujitambulisha na kama wao ni wachache basi wape nafasi wajitambulishe au kama mwafahamiana basi anza na mada
c) wakati wa presentation usisimame wima kama mlingoti, hii huongeza stress kwani misuli na damu havishughuliki sana, tembea tembea, angila kona tofauti na endelea kutoa mada taratibu
d) Hakikisha unashirikishana vema na unaowapa mada kwa kuuliza maswali, kuomba extra comments,nk
e) Chagua "cheerleaders"(sijui niwaitaje) :katika presentation lazima kuna watu wanafuatilia kwa makini labda wanatikisa vichwa au kusmile ukitoa point fulani hawa ndio tunawaita cheerleaders ktk presentation;Utapojihisi unakosa confidence pata courage fro these cheerleaders na amini kuwa hata kama kuna kitu nakosea kidogo basi kuna watu wanafurahia presentation yangu.
f) Tumia body language vizuri: kama unaelezea janga linaloikumba kampuni huwezi kucheka cheka, body language ionyeshe kweli nawewe umeguswa na janga hilo. Kama unaeleza sera mpya za kampuni pia utaonyesha userious fulani,na kama unaleza jinsi kampuni ilivyovuka malengo kwenye mauzo na kukamata wateja wengi hakika hapo uso wako utakuwa excited kwani ni habari ya neema kwa kampuni. Huwezi kusema "ninafuraha kuwaeleza mafaniko makubwa tuliyopata mwaka jana" huku umenuna na uso umejikunja,audience wanaona body language inavyopingana na maelezo yako
g)Amini kuwa unaweza na kila presentation iwe bora kuliko iliyopita: remember the rule of thumb "Practise makes perfect"
my take:
ktk society yetu public speaking imekuwa ni tatizo sana, tu wasomi, tu nadhifu but we cant speak our thoughts out. Basi tuanze kwa watoto, tuwajengee mazingira ya kujiamini-hata kumpa mtoto akueleze jinsi alivyospend siku yake yatosha.
Na shule zetu ziwape changamoto watoto kwa midahalo na majadiliano.