Nini husababisha watu wasirudi hospitali kurudia vipimo kuhakiki kama wamepona?

Rule L

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
1,846
Reaction score
2,754
Kama nilivyoeleza hapo juu.

Ni kwanini watu wengi sana wanapoenda hospitali kutibiwa na kisha kuambiwa warudi kuhakiki vipimo iwapo wamepona hua hawarudi?

Hupewa muda pengine baada ya wiki moja au mwezi warudi ila walio wengi hua hawarudi hata kama hakuna gharama za ziada.

Je, wewe kwako hili lipoje? Kwangu mimi nikitumia dozi nikajiona niko fiti hua sirudi.

Kwasababu naona ni kupoteza muda na kubana nafasi ya wengine kutibiwa.
 
hatuna utamaduni huo. Lazima kuwajengea watu tabia ya kufuatilia vipimo.
2. Pesaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa...hili nalo ni contributing factor kubwa among many
 
Binadamu tulivyo..kama haiumi, haijavimba na haimzuii kufanya shughuli za kila siku sio rahisi akaona umuhimu wa kurudi

Pili, gharama za hospitali
 
๐Ÿ™„
 
Hio dozi tu kumaliza kwa mbinde
Ukinywa vidonge vyako siku 1 ukapata nafuu ndio imeisha hioo ๐Ÿ˜…
Hili nalo waliangalie Kuna kipind ndani kwangu kulikuwa kama pharmacy kias Kwamba nduguzangu wasio na bima wakiandikiwa dawa hospital wanakuja stock kwanza kucheck km hakuna ndo wanunue๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Sababu.
1. Elimu duni juu ya naswala ya afya
2. Gharama kubwa za matibabu
3. Umbali wa huduma inapotolewa
4. Usumbufu/mchakato mrefu wa upatikanaji huduma
 
Hili nalo waliangalie Kuna kipind ndani kwangu kulikuwa kama pharmacy kias Kwamba nduguzangu wasio na bima wakiandikiwa dawa hospital wanakuja stock kwanza kucheck km hakuna ndo wanunue๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
nikutukane au nikuache...????
 
Mambo ni mengi muda mchache. Ukijihisi una afadhali kidogo tu unajiona ushapona unawahi kwenye harakati zako pia nahisi yale mazoea ya kujiona kila mtu ni daktari kupima kwa kutumia macho tu nayo inachangia sana
 
Kama umepona, kurudia vipimo na nyomi za wagonjwa ni sawa na kumjaribu Mungu.
Kama hujapona unakwenda kwingine, Kwa nini Urusi kwa aliyeshindwa na utozwe gharama nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ