Nini itasaidia kuepusha vipigo na mauaji baina ya wanandoa?

Nini itasaidia kuepusha vipigo na mauaji baina ya wanandoa?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
NINI ITASAIDIA KUEPUSHA VIPIGO NA MAUAJI BAINA YA WANANDOA?

Mwanamke hii inaweza kukusaidia mwanamke Kijana ambaye unaingia Ndoani.

1. Hakikisha kabla hujaolewa uwe na Elimu sahihi juu ya Ndoa.

2. Unapoamua kwamba unataka kuolewa hakikisha unatafuta nguvu hizi tano ziwe kwako.

i. Nguvu ya Imani
ii. Nguvu ya Akili
iii. Nguvu ya malezi
iv. Nguvu ya Mapenzi na
v. Nguvu ya Uchumi

3. Unapoamua kuingia ndoani hakikisha unaolewa na mtu unayempenda nasio mtu wa kufanya maisha. Olewa na mtu anayekupenda lakini sio wa kufanya maisha (Hii inaeleweka)

4. Ishi Uanamke, yani Usipoteze Uanamke wako kwa gharama zozote zile. Ni kigezo kikubwa cha kuepusha mengi.

5. Ndani ya ndoa usitembelee madonda ama maumivu ya mahusiano uliyoyapitia zamani.
 
Kiukweli naanza na malezi .

Wazazi tumezoea kusema, mtoto wa kiume halii, mtoto wa kiume unalalamika lalamika kutwa. Kumbe inatakiwa turuhusu wanaume wawe expressive tangu utoto. Mwanaume akisema kinachomkera nadhani itasaidia. Sasa unakuta mwanamke kamkera mkaka.

Kaka hasemi anagugumia tu anaweka kinyongo. Siku mwanaume anakuja kuwa triggered kidogo tu basi🙌🙌 anamlabua mtu risasi.

Na kingine natupa lawama kwa makungwi. Hawa wanawafunda wadada wawaabudu wanaume sasa na sio kuishi nao kama waume zao. Nadhani tuanzie hapo.
Mtu anakwambia mwanaume mnyenyekee sasa unakuta mwanaume mwengine akinyenyekewa wakati alipotoka alikua andharaulika badi anajikuta mungu mtu anavaa umungu na kuanza kumnyoosha yule dada ili ku prove superiority yake.

Na kingine wanakwambia mwanamke usimfatilie mumeo🤣 unaishi kwa adabu miaka 20 unakuja kustuka baada ya miaka 20 mume kakuzalia watoto sita nje wanahamia kwako🤣🤣yote hiyo ulikua hutaki kufatilia. Jamani🤣
 
Back
Top Bottom