superwarkills
Senior Member
- Aug 18, 2014
- 136
- 83
Vipi siku akiitwa hivi kiongozi mkubwa mbele ya kadamnasi atakubali likae kifuani au ndiyo ataswaga mtu..kwa kuwa ni neno la msimu..Haya huwa ni maneno ya msimu tu hupita
Kupe limekuwa likitimika Kwa muda mrefu, sidhani kama kuna aliyejisumbua kutoa ufafanuzi. Maana inaeleweka, hata ikiwa anayehusishwa ni mtu.Ndugu wadau hivi karibuni kumekuwa na matumizi makubwa sana ya neno chawa,najua chawa halisi (waliowafuga) wengi mnawafahamu ,je ni sawa jamii kuitana chawa ili hali chawa ni mdudu.
Tafsiri isiyo rasmi mtaani wanasema chawa ni kama mpambe na kiaina kama kuwadi hivi. Je ni kweli..basi
BAKITA watupe tofauti ya neno MPAMBE na CHAWA ni lipi sahihi kwa matumizi ya sasa na kwa nani ?
Nafikiri hasa neno chawa kutumika kuwakilisha "wapambe" inatokana na tafsiri ya neno la kiingereza la "parasite" yaani kiumbe ambaye hawezi kuishi bila kutegemea kiumbe mwingine!Ndugu wadau hivi karibuni kumekuwa na matumizi makubwa sana ya neno chawa,najua chawa halisi (waliowafuga) wengi mnawafahamu ,je ni sawa jamii kuitana chawa ili hali chawa ni mdudu.
Tafsiri isiyo rasmi mtaani wanasema chawa ni kama mpambe na kiaina kama kuwadi hivi. Je ni kweli..basi
BAKITA watupe tofauti ya neno MPAMBE na CHAWA ni lipi sahihi kwa matumizi ya sasa na kwa nani ?
Maana yake ni ipi mkuu?Kuna maneno mengi tu ya kiswahili yamepotoshwa maana yake halisi...mfano mzuri ni neno "Ngono" linavyotumika sasa sio maana ya matumizi yake halisi kwenye kiswahili.
Nilimsikia mtaalam mmoja wa Bakita akisema maana halisi ya neno "Ngono" ni kuwa hufanywa na wanawake zaidi ya mmoja waliiolewa na mume mmoja almaarufu "mitala" sasa zile zamu wanazopeana kulala na mume wao ndio inaitwa ngono! kwa hiyo yeye binafsi anasema akisikia watu wanasema ameshiriki ngono zembe huwa anafikiri mwanamume yule alilala na mkewe mwenye zamu bila ya chandarua hahahaah!Maana yake ni ipi mkuu?