Nini kifanyike ili kutokomeza rushwa na ufisadi?

Pac the Don

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2021
Posts
6,170
Reaction score
7,710
Kumekua na jitihada nyingi ingawa sio halisi za kupambana na ufisadi mpaka ukaundwa Mahakama ya mafisad! Binafsi naamin katika sheria kali ambazo zitapatikana kupitia katiba mpya.

Hatuwez kamwe kupambana na ufisadi, rushwa na ubadhirifu wa mali za umma kwa mfumo huu wa utawala na katiba iliyopo. Kibaya zaid anaepigana na ufisadi ndio wa kwanza kuwapa kinga supika plus jaji!! Nchi hii uzalendo bado sana!

 
Yesu arudi labda.

Utamaduni wa ubinafsi ndio chanzo cha kila kitu, kila mtanzania ni mpenda rushwa pale anapopokea au kunufaika nayo.

Tunaichukia rushwa pale inapotuumiza tu. Rushwa tunaipenda mno wadanganyika kiasi kwamba imetamalaki kunzia viunga vya Ikulu mpaka kwa mjumbe wa makumi.
 
Well, but tatizo ni kwamba hatujaweka misingi imara ya kusimamia tatizo hilo, cz ikiwepo mifano ya viongoz wakishughulikiwa kusawasawa kwa sheria kali, ita reflect kwa wananchi nao wataogopa kufisadi maan wanaona viongoz wakifungwa maisha gerezani!!
 
Hakuna uwajibikaji than sheria kali, hakuna!! Ndo maan vitabu vya dini kuna sheria, mataifa yote kuna sheria ili kumuwajibisha mkosaji!! But not akili kwamba itasaidia hilo
Umeielewa hiyo maana ya akili ?
 
Tiba Bora sio katiba mpya pekee, tuanze matumizi ya Artificial intelligence kuanzia mashirika ya kiserikali kama TRA, TAKUKURU, TBS.
 
Ufisadi na rushwa utatokomezwa kwa kuunda sheria kali na pia kwa wale wanaoombwa rushwa wakiweza kureport wapewe bakshishi kama asante maana itasaidia kuibua mambo hayo na pia kutokomeza kabisa.
 
Hakyii ya Murhunguuu/Ruwa rushwa haitokaaa iiishe katika uso wa Dunia hiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…