Glady michael
Member
- Aug 9, 2022
- 13
- 13
Makala yangu imejikita zaidi katika kuelezea makosa ambayo hufanywa na wafanyabiashara wengi na hata watu ambao huanza kupanga kufanya biashara. Makosa hayo hufanya watu kudidimia Baraka ya kufanikiwa. Je nini kifanyike? Tutaona mbinu, njia, au mwongozo ambao ni muhimu kufuata ili ufanikiwe kiuchumi kwenye biashara.
Kwa kuanza na makosa tunaona makosa hayo kama ifuatavyo:-
1. Kutomtanguliza MUNGU katika mipango yako au katika biashara yako na kufanya unavyotaka pasipo kumshirikisha.
2. Mipango mibovu katika biashara yako kwa kwa biashara unayoitaji kuifanya.
3. Uoga na kutothubutu kutenda kile unachoitaji kufanya au kwa mfanyabiashara kutangaza kile anachofanya.
4. Tamaa na ulimbukeni katika biashara.
5. Dharau, chuki, kiburi, kejeri, uhasama, na ubinafsi katika biashara.
6. Mazingira mabovu au ambayo sio sahihi katika biashara.
7. Ukosefu wa fikra katika kubadili mikakati au njia nyingine mbadala za kuboresha biashara na badala yake kusimama katika njia moja.
8. Matumizi mabaya ya faida inayopatikana kwa mfanyabiashara.
9. Mawazo potofu kwa mfanyabiashara kwa kile anachokifanya.
10. Kukata tamaa mapema mno katika biashara.
Je nini kifanyike ili uweze kufanikiwa katika biashara yako na kuiona muhimu na ndio ndoto yako katika kukupatia kipato na maisha bora. Zifuatazo ni njia sahihi za kufuata kwa mfanyabiashara yoyote yule ili aweze kutoboa zaidi au kwa wale wanaohitaji kuanza biashara, hizi ndio njia pekee kumi.
1. Kutomtanguliza MUNGU katika mipango yako na biashara yako. Kuna watu katika kupanga mipango yao ya biashara ni ngumu sana kumshirikisha Mungu mpaka pale akiona amekwama ndio huona Mungu yupo. Ndugu yangu hakuna kinachofanikiwa bila Mungu. Mungu ndiye njia yako kuu na wa kwanza katika mipango yako, hakika utafanikiwa.
2. Kuwa na nguvu ya kuthubutu na kuondoa uoga kwa kile unachokifanya. Watu wengi wanahitaji kufanya biashara lakini tatizo lao kubwa ni uoga na kutojiamini kwa kile anachotaka kukifanya. Unakuta mtu ni mfanyabiashara lakini hapohapo ni muoga na hajiamini katika biashara yake. Kwa mfano unakuta wauza mitumba labda ana nguo zake mahali anaona kabisa wateja hawafiki lakini ukimshauri akatembeze anaweza kusema ohoo watu watanionaje huko mtaani sitaki wajue kama nauza mitumba! Punguza uoga na jaribu kufanya kweli kwenye biashara yako. Na kama waitaji kufanya biashara basi acha mara moja tabia ya uoga.
3. Kuwa na mipango sahihi na dhabiti kwa kile unachokifanya au unachohitaji kukifanya. Kuna watu hukosa mipango sahihi kwenye biashara zao. Kwa mfano wanaofanya biashara ndogondogo tuseme vitafunio, mtu huyu biashara yake inaweza kumfanya asogee maeneo mbalimbali kutembeza lakini yeye mpango wake ni mmoja tu kukaa nyumbani kuuza alafu biashara isipoisha atalalamika karogwa au mkosi. Kuwa na mipango dhabiti kwenye biashara yako.
4. Kuacha tamaa na ulimbukeni katika biashara na kuheshimu biashara yako. Tuseme ukweli wafanyabiashara wengi hushindwa kufika mbali hii ni kutokana na tamaa zao walizonazo katika biashara na kusahau kuwa anachokifanya sasa hivi ndio alichopanga awali. Kwa mfano unakuta mtu anauza genge hapohapo anatamani duka kama la rafiki yake na kusahau kuwa pale kwenye genge hajafanikiwa hata robo mwishowe atazembea na kuanguka kabisa. Pia heshimu kile ulichonacho maana haujui lini kitakunufaisha na uache tamaa kwa vitu ambavyo huna uwezo navy’s.
5. Kuwa na njia tofauti tofauti katika kuboresha biashara yako. Pia ili uweze kufanikiwa lazima upambane kwa njia tofauti tofauti, sijasema ubadili biashara Hapana! Bali jaribu kuwa na njia tofauti za kukuwezesha kuimarisha na kuboresha biashara yako na sio kuwa katika njia moja tu, namaanisha ukiona njia moja imeferi basi jaribu nyingine. Kuna njia nyingi sana za kufanikisha biashara yako. Kwa mfano kuna kufanya delivery, kutembeza, kutangaza mitandaoni hata kwa njia ya mikopo. Iwe inaendana na biashara ipi unafanya au unahitaji kufanya.
6. Kutokukata tamaa mapema Kabisa katika biashara yako. Ewe mfanyabiashara jaribu tena na tena na kuacha kukata tamaa kwa kile unachokifanya kwani hakuna kinachoshindikana chini ya jua, hakika utafanikiwa.
7. Boresha mazingira katika eneo la biashara yako. Watu wengine biashara zao haziendi kutokana na maeneo waliyopo hasahasa wafanyabiashara wadogo. Ili kuvuta wateja kwa wingi ni bora uweke mazingira safi na kuwa msafi binafsi hii ni njia pekee ya kukuongezea wanunuzi katika biashara yako.
8. Ondoa chuki, dharau, uhasama, uadui, kejeri, hasira, na majivuno katika biashara. Kama unaitaji kufanya biashara basi kama una tabia hizi acha mara moja. Na kama wewe ni mfanyabiashara huna budi kuachana na tabia hizi kwani ndio chanzo cha kudidimia kwa biashara yako. Shindana kwenye biashara kwa amani na utulivu wa fikra pasipo uadui au uhasama na wenzako. Kwa mfano kurogana, ndugu yangu hakuna kisicho na mwisho leo utafanikiwa kesho utadidimia jitahidi ufanikiwe kwa amani.
9. Punguza mawazo potofu na njia hasi katika biashara yako. Kuna baadhi ya wafanyabiashara hawaamini kile wanachofanya nakuona kama masihara hii ni kutokana na mawazo yao potofu ya kutofanikiwa. Ndugu yangu jipe moyo wa kushinda na kufanikiwa mda wote kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha.
10. Njia ya mwisho kabisa jiajiri. Tafuta mtaji, fikiri, panga, pendekeza, anza kutenda au chukua hatua, na mwishowe wekeza kwa unachokipata na kuwa na matumizi mazuri ya faida yako hakika utafanikiwa.
Hitimisho: chanzo cha umaskini wako ni wewe mwenyewe na mabadiliko huja baada ya kazi. Boresha biashara yako ewe mfanyabiashara, kama unaanza anza kwa hizo kanuni. Kijana usisubiri kuajiriwa mikono yako ndio ajira yako kwa Tanzania hii. Wekeza kijana

Upvote
0