dour
Member
- Aug 7, 2017
- 7
- 9
UTANGULIZI.
Utawala bora ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, kidemokrasia, kijamii na hata maandeleo ya mtu mmoja mmoja. Utawala bora ni zoezi la viongozi katika ngazi zote kusimamia misingi ya haki na usawa katika matumizi ya rasilimali kwajili ya maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Utawala bora unapaswa kuzingatiwa katika ngazi zote za uongozi kuanzia kitongoji, kijiji, halmashauri hadi ngazi ya kitaifa. Utawala bora unapaswa kusimamia misingi ya uwajibikaji, uwazi, haki na usawa, utawala wa sheria, ushiriki pamoja na kutatua migogoro kwa mujibu wa sheria na utaratibu.
Kumekua na utaratibu wa viongozi wa ngazi za juu na kitaifa katika mikutano kutatua migogoro ya wananchi moja kwa moja, migogoro ambayo ingepaswa itatuliwe na mamlaka zenye wajibu. Kumiminika kwa wananchi katika hadhara kwa kigezo cha kutatuliwa changamoto ni wazi bado hali ya utawala bora ni ndogo sana. Katika ripoti ya CAG bado kuna taarifa za rushwa na ubadhilifu kwenye ngazi za uongozi. Hii ikiashiria bado hali ya utawala bora katika nchi yetu ipo chini
Kwakua tunahitaji maendeleo ya kweli na kutokomeza umasikini, utawala bora ni sehemu ya kwanza tunayo paswa kuitizama kwa kina. Kwa tanzania niitakayo, yafuatayo ni mapendekezo yangu ili kuboresha hali ya utawala bora nchini.
1. Utumiaji wa teknolojia za kidijitali katika ngazi za uongozi.
Katika mapinduzi haya ya teknolojia ya kidijitali yatupasa kutumia kikamilifu ili kuweza kuboresha uwazi na ushiriki. Napendekeza kuanzishwa kwa website za kila kata ambayo itakua mahsusi kwa taarifa za msingi za kiuongozi. Kufanya hivi kutaimarisha ukweli na uwazi baina ya viongozi na wananchi. Katika website hiyo kuwekwe mapato na matumizi ya kata, tenda pamoja madawati mbali mbali ya malalamiko ikiwemo ya ardhi, takukuru na dawati la jinsia.
Matumizi ya teknolojia mpya ya akili mnemba kuweza kuboresha ubora wa taarifa katika uwajibikaji na utoaji taarifa kwa umma. Napendekeza kuanzishwe chatbot mbalimbali katika kupata taarifa za msingi. Matumizi ya teknolojia ya block chain katika kudhibiti kufoji na kubadili taarifa za miamala. Matumizi ya teknolojia ya IoT(internet of thing) katika kukusanya kutunza na kusambaza taarifa.
Napendekeza uanzishwaji wa majukwaa ya ushiriki ya umma kwa kila kata. Majukwaa ambayo wananchi watashiriki moja kwa moja kwenye majadiliano huku viongozi wakiwemo. Ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi unaleta taswira ya kweli ya demokrasia. Mfano wa majukwaa nikama ya telegram, wasap pamoja na majukwaa mtandao.
2. Kuanzishwa kwa mahakama za viongozi.
Viongozi wengi ambao wanabainika katika ubadhilifu huishia kutenguliwa tu au kupangiwa majukumu mengine hali ambayo inachochea ubadhilifu na uzembe. Napendekeza kuanzishwa kwa kwa mahakama ya viongozi. Viongozi ambao watabainika kuvunja misingi ya utawala bora washitakiwe na kupewa adhabu stahiki. Napendekeza matangazo ya mienendo ya kesi za viongozi irushwe mubashara ili wananchi waweze kufuatilia na iwe funzo kwa viongozi wengine.
3. Uanzishwaji wa ratiba ya utatuzi wa changamoto kitaifa.
Inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wakuu wa kiwilaya na kimkoa kutotembelea kabsa maeneo wanayo yasimamia wakisubiri changamoto za wananchi ziwafuate ofisini. Napendekeza kuwa na ratiba ambayo viongozi wote wa kimkoa watakutana na wananchi wao katika kata zao na kutatua migogoro mbali mbali inayo wakabili wananchi. Kufanya hivi kutaongeza haki na usawa kwa wananchi.
4. Dawati la wajumbe wa takukuru kila kata.
Ili kutokomeza rushwa kutoka ngazi ya kitongoji napendekeza kuanzishwe dawati la rushwa ambalo litakua na mjumbe mwakilishi kutoka takukuru, wajumbe hawa watasambazwa kila ofisi ya kata. Mjumbe huyu atakuwa na mawasiliano ya wazi wa wananchi kupitia namba ya simu. Kufanya hivi kutarahisisha zaidi utoaji wa taarifa zinazohusu rushwa na ubadhilifu. Hii itaongeza uwajibikaji ambayo ni msingi wa utawala bora.
5. Kutokomeza ubaguzi wa uchama katika utendaji.
Tunapokuja kwenye swala la kujenga uchumi na maendeleo tumeona baadhi ya watendaji wenye weledi kuachwa sababu ni wa chama kingine, hivyo kupelekea kupata watendaji wa serikali wasio na welidi kwa kigezo cha chama kimoja. Moja kati ya malalamiko makubwa ni wawakilishi wa baraza la usuluhishi la ardhi kata kulalamikiwa kuwa na watendaji wasio na weledi. Kupata viongozi wenye weledi kutaongeza ufanisi katika usimamiaji wa taratibu na haki.
6. Majukumu ya viongozi yawekwe wazi.
Idadi kubwa na wananchi hawajui majukumu ya viongozi na watendaji wao. Yamo malalamiko katika ngazi zakata kuombwa mchango wa wino wa muhuri. Wengine wakitatuliwa changamoto na viongozi kwa fedha wakati ni majukumu yao. Majukumu ya viongozi yakiwekwa wazi yatatoa taswira nzima ya uongozi na hii itaondoa rushwa kwa kiasi kikubwa maana wananchi watakua wanajua taratibu za kufuata kupata haki zao.
Kwa ujumla zinahitajika jitihada kuleta utawala bora, serikali kupitia tume ya haki na utawala bora iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu ya viongozi. Serikali iboreshe mifumo yao ya usimamizi katika minyororo ya madaraka, kuboresha usimamizi katika minyororo ya kimamlaka kutaleta utawala bora zaidi.

Upvote
6