Nini kifanyike kukomesha biashara ya dawa za kulevya nchini?

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kila mara tunasikia taarifa za ukamataji mkubwa, operesheni nzito na kampeni za kupambana na dawa za kulevya… lakini mitaani mtandao wake unazidi kuenea.

Je, tatizo ni udhaifu wa mifumo ya sheria? Ni viongozi hawawajibiki ipasavyo? Au kuna watu wenye nguvu wanaonufaika na biashara hii?

Kila siku tunavyonyamaza, vijana zaidi wanapotea, familia zinavunjika, na taifa linapoteza nguvu kazi.

Unadhani kawanini watu wanafanya hii biashara licha kuwa na adhabu kali?

​
 
I'm in my black benz
Doin' cocaine with my black friends -juice wrld
 
Watumiaji waache kutumia tu. Biashara ikikosa wateja itajifia yenyewe
Chenye Watumiaji Kamwe Hakiwezi Acha Kutumiwa...Wayaruhusu Tu....Hivi Wanavyo Yabana Ndio Wanayaongezea Thamani Zaidi...Na Utafutajwi Zaidi....
 
Watu wanachangia bilion 10 kwenye chama unatagemea watu kama hao ni biashara gani inawaingizia mahela yote hayo, na kwanamna hiyo serikali ni kama imetiwa mfukoni
 
Kwa ushauri wa fasta fasta
●Serikali ianze na bodaboda haw watu ni drug deals wakubwa kwa macho ya kawaida ukiwaona unaweza kusema ni bodaboda lkn sio wanasafirisha madawa kila siku
● lkn pia hii biashara niyawakubwa na wapo seikalini nazani wafanyiwe uchunguzi wa kina waheshimiwa
● wasanii wa mziki hawa nao ni mawakala wa usambazaji madawa unkuta msanii ktwa anasafiri nje ya nchi et kwebmnda kula bata hao wanakuwa wamebebeshwa madawa
● Rushwa bado ni tatizo maana tz do inaongoza kama njia ya madawa kwenda south africa kwaio
 
Hii biashara haiwezi kuisha

Ova
 
Kama kina zungu wataendelea kushinda uchaguzi tusahau vita hiii
 
Tusijichoshe. Hamna vijana wanaopotea kwa idadi ya maana. Labda kama unazumgumzia madawa ya pombe na bangi.
 
Tanzania hakuna uzalendo ndugu yangu. CCM wanapigania ulaji wao na watoto wao. Dawa za kulevya zikiua mtoto wako, wao vigogo wa CCM wanapungukiwa na nini wakati watoto wao wapo salama??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…