SoC04 Nini kifanyike kukuza ubunifu wa teknolojia kwajili ya maendeleo ya taifa kuendana na kasi ya dunia

SoC04 Nini kifanyike kukuza ubunifu wa teknolojia kwajili ya maendeleo ya taifa kuendana na kasi ya dunia

Tanzania Tuitakayo competition threads

dour

Member
Joined
Aug 7, 2017
Posts
7
Reaction score
9
UTANGULIZI.
Ubinifu wa teknolojia umeendelea kushika kasi dunia huku gunduzi za teknojia mbalimbali zikigunduliwa kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo mawasiliano, elimu, afya, usafiri za uzalishaji. Teknolojia ni mchakato wa utumiaji wa maarifa ya sayansi kwa dhumuni la vitendo au matumizi. Teknolojia ina umuhumu mkubwa katika maendeleo ya taifa katika uchumi, kidemokrasia na kihuduma. Kumekua na mifano mingi ya mapinduzi ya teknolojia duniani ikiwemo ugunduzi wa akili mnemba pamoja na ugunduzi wa mifumo ya kieletroniki.

Ubunifu wa teknolojia ni mchakato ambao unawezesha upatikanaji wa teknolojia mpya au iliyoboreshwa na kusambazwa ili kuwafikia walengwa. Ingawaje bunifu mbalimbali huzalishwa katika taifa letu hua hazipigi hatua na nyingine nyingi zikipotezewa na kupotea. Hali ya ubunifu nchini inaendelea kukua taratibu ingawa inakutana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa rasilimali na miundombinu, ukosefu wa sera ambazo zinahamasisha ubunifu, upungufu wa elimu katika jamii.

Katika kufikia Tanzania tuipenda ndani ya miaka 5 hadi 25 natamani kuona teknolojia zetu tulizobuni zitusaidie kwenye uzalishaji na kuuza teknolojia zetu kwenye nchi mbalimbali. Ili kufikia Tanzania tuitakayo katika ubunifu wa teknolojia napendekeza yafuatayo yafanyike.

1. Uboreshwaji wa sera zitakazochochea ubunifu.
Ili kukuza ubunifu katika teknolojia wizara ya sayansi na teknolojia inapaswa kuunda sera madhubuti ambazo zitasaidia kukuza ubunifu. Sera hizo zinatakiwa kusisitiza utengwaji wa bajeti katika wizara ili kuchochea ubunifu, sera ya ununuzi na matumizi ya teknolojia uliobuniwa tanzania, hatimiliki za wabunifu, pamoja na sera za wazi kupata data kwa watafiti.

2. Uanzishwaji wa tuzo zenye hadhi kwa wabunifu.
Katika utambuzi na kuchochea ubunifu tunapaswa kuanzishwa kwa tuzo mbalimbali za ubunifu. Tuzo hizi ziwekwe kwenye historia ya taifa kama watu wamsingi wa taifa hili. Tuzo hizi zitakuza ushindani na ubunifu wenye tija pamoja na kuunganishwa kwa wabunifu mbalimbali katika taifa hili. Mataifa yaliyo endelea wana tuzo zao kubwa za ubunifu katika teknolojia mfano tuzo za nobel. Tuzo hizi zitavutia wawekezaji na kusaidia wabunifu kupata ufadhili katika tafiti zao.

3. Mfumo wa wazi wa utumaji tafiti za ubunifu uboreshwe.
Japokuwa kumekuwa na mfumo wa ubunifu "ubunifu portal" lakini watanzania wengi hawana ufahamu kuhusu mfumo huu. Napendekeza mfumo uboreshwe zaidi uwe na lugha rafiki kwa kila mbunifu aweze kutuma ubunifu wake. Napendekeza kila taasisi ya elimu ya juu kutoa tafiti tano bora kila mwaka tafiti hizi zitangazwe na ziwekwe kwenye mfumo huu ambao tutapata mawazo ya kibunifu.

4. Serikali kutoa mitaji kwa wafanya tafiti mbalimbali katika halmashauri.
Kufanya tafiti ni gharama sana kiasi ambacho wabunifu wengi hufeli wakati wa tafiti. Kama ambavyo serikali hutenga 10% kwajili ya wajasiriamali, napendekeza serikali itenge asilimia kadhaa angalau 2% katika halmashauri zetu kwajili ya kuwezesha wafanya tafititi mbalimbali kufanya tafiti zao za kibunifu.

Uwekezaji ni kitu cha msingi katika kukuza bunifu katika teknolojia. Serikali kupitia tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) ishirikiane na mashirika binafsi yanayo saidia vijana katika ubunifu mfano "tryEngineering" yaweze kuwekeza kwenye ubunifu. Serikali na mashirika binafsi yatafute bunifu mbalimbali mtaani kwakuanzisha "ubunifu serch" hii itasaidia kukuza mawazo ya kibunifu.

5. Kuanzishwa na kuboreshwa kwa taasisi mbalimbali zinazobadili mawazo bunifu kuwa uhalisia.
Tunapaswa kua na wataalam kama wahandisi na wana IT mbalimbali ambao watachukua mawazo bunifu kuyachakata na kubadili kwenye uhalisia. SIDO imeonekana kua msaada kwenye kubadili mawazo ya kibinifu kutengeneza uhalisia. Napendekeza maboresho pamoja na kutengewa fedha ili kutimiza jukumu hili. Ushirikiano wa taasisi binafsi katika utekelezaji huu unapaswa kuzingatiwa.

6. Ulazima wa somo la TEHAMA katika ngazi zote za elimu.
Katika ukuaji wa teknolojia ya tehama sasa hutumika kwenye kila nyanja za uzalishaji na taasisi zote za utendaji. Kunao umuhimu mkubwa sasa wa kufanya somo la tehama kua la lazima katika ngazi zote za elimu. Serikali inapaswa kutoa mwongoza, kutenga bajeti kubwa itakayo saidia kununua vifaa na walimu ambao watafundisha ili somo kwenye kila ngazi ya elimu.

7. Ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika kutangaza ubunifu.
Umuhimu wa wa vyombo vya habari katika kuelimisha na kutangaza teknolojia zetu ni mkubwa sana. Napendekeza katika chaneli zetu kuanzishwe vipindi mbalimbali vya kutangaza teknolojia zetu, na kuelimisha umuhimu wa ubunifu katika kukuza taifa lenye maendeleo kwenye kila nyanja pamoja na historia za mafanikio ya wabunifu mbalimbali.

HITIMISHO.
Kwa ujumla kuhamia katika taifa lenye uwekezaji katika ubunifu wa teknolojia inawezekana, serikali ishirikiane na wadau mbalimbali ikiwemo wananchi katika kitatua changamoto zilizopo ili kufikia tanzania tuitakayo inayojitegemea kiteknolojia. Ubunifu ni zao la uimara wa elimu na uthubutu hivyo kwapamoja tuthubutu katika kuleta maendeleo ya kibunifu ya teknolojia. Ubunifu ni nguzo ya maendeleo, tusipo kubali kubuni vyakwetu tutaendelea juu ya migongo ya mataifa mengine.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom