Nini kifanyike kupunguza ajali za malori ya masafa marefu zinazosababishwa na uchovu mwingi kwa madereva?

Nini kifanyike kupunguza ajali za malori ya masafa marefu zinazosababishwa na uchovu mwingi kwa madereva?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Ajali nyingi zinatokea zikihusisha malori kama umechunguza mara nyingi huwa ni sababu dereva alisinzia kutokana na uchovu mwingi wa kuendesha muda mrefu bila kupumzika au anakuwa ametumia vilevi, na mbaya zaidi anakuwa peke yake.

lorii.PNG

Licha ya sheria kuwataka kuwa madereva wawili ili kukabiliana na uchovu unaweza kumnyong'onyesha dereva akiwa peke yake, lakini pia wasitumie pombe wawapo kazini, hili halionekani kufuatiliwa, jambo linalosababisha tupoteze nguvu kazi za taifa kila kukicha.

Je, unadhani nini kifanyike kukabiliana na hili?

 
Hongezeni mshahara tu maana we ukipanda gari lisaa limoja unasinzia wakati dereva anakaa macho Masaa nane kazi ngumu hii
 
Madereva wawili kwenye gari moja uchovu si ule ule? Uber wamefanikiwa kupitia teknolojia. Bunduma ajifunze huko
 
Dawa ni dereva Mwenyewe kujihisi amechoka aegeshe pembeni Apige usingizi/apumzike
 
Madereva wawili kwenye gari moja uchovu si ule ule? Uber wamefanikiwa kupitia teknolojia. Bunduma ajifunze huko
Umeenisha nini hapa Mkuu? Masaa yakiisha dereva anaondolewa kwenye mfumo au?
 
Madereva wanapumzika sana njiani ni wa malori. Ukitoka tu unawakuta Chalinze wamepaki, kila mji (miji midogo ya barabarani) utakuta malori yamepaki.
 
Suluhisho la ajali za barabarani ni kuongeza treni za mizigo na abiria kama ilivyo kwenye mataifa yaliyoendelea.
Tukitumia usafiri tofauti na mabus au malori tutaepusha ajali nyingi Sana
 
Kutokana na Jambo hili mm naihasa Sheria ya usalama WA barabarani ifuate Sheria yake ili madereva wawe na tahadhari juu ya uwendeshaji wa magari ktk barabara ikitokea driver ambae amelewa na askari wakijua kama dereva huyu kasababisha ajali akiwa amelewa basi naviomba vyombo vya Sheria vichukuwe mkondo wake ikiwemo na kuwatonza faini kubwa ili iwe fundisho Kwa taifa Kwa ujumla
 
😡😡hawa dawa yao ni kujichukulia sheria mkononi.
Tunashuka apo Zambia tunawaonesha kila rangi
 
Back
Top Bottom