Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi huadhimishwa Februari 11 kila Mwaka kuadhimisha mafanikio na michango ya Wanawake na Wasichana katika Sekta ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM)
Siku hii inahamasisha Wanawake na Wasichana zaidi kufuata na kujiunga na taaluma za Sayansi na Teknolojia lengo likiwa ni kuvunja vizuizi na dhana potofu ambazo Kihistoria zimezuia Ushiriki wa Wanawake katika sekta hizi
Utafiti wa mwaka 2022 ulionesha kuwa mwanamke mmoja kati ya wawili walioko katika fani ya Sayansi wameripoti kukutana na unyanyasaji wa kijinsia kazini.
Licha ya upungufu wa ujuzi katika maeneo mengi ya kiteknolojia, wanawake bado wanachukua asilimia 28 tu ya wahitimu wa masomo ya Uhandisi na asilimia 40 ya wahitimu katika masomo ya sayansi ya kompyuta.
Chanzo: United Nations