Nini kifanyike kuzuia uonevu mashuleni?

Nini kifanyike kuzuia uonevu mashuleni?

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Shule zote zina watu ambao huonea wengine iwe kwa matusi, vipigo, vitisho, uharibifu, ngono n.k.

Athari za huu uonevu ni mkubwa sana kwa anayeonewa, Wazazi hatukai na watoto na kujua nini kina waathiri au nani huwaonea.

Je, tufanyeje kuondokana na hii hali?

NB:. Binafsi nimemwambia mtoto, sitaki aje kachaniwa madaftari, au kanyanganywa kitu fulani, sitaki aje aseme amepigwa.

Akichaniwa daftari yeye naye achane. Akipigwa ampige aliyempiga

Na nimewaambia na walimu wake pia kuwa mi nishamfungulia wangu, akiguswa atawagusa wamgusao.
 
Ni sawa unavyosema ila kila jambo lina pande mbili faida na hasara vipi wakimshawishi kuingia vitendo vya kishoga aingie wakimgusa makalio awaguse waendeleee?
 
Ni muhimu mtoto umfanye awe huru kukuambia na kukupa taarifa zote ya kile kilichojiri.

Kumwambie asije kushtaki ni kuzuia Baadhi ya taarifa muhimu na nyeti Kwa mtoto wako.
Ni kukimbia majukumu.

Mwambie asionewe kizembe lakini aje kusema Kama kunashida yoyote imetokea.

Msisitize mtoto kuwa hutokubali kusikia yeyote anamnyima haki zake. Mwambie wewe ndio Baba yake hivyo upo Kwa ajili yake kumlinda.

Pia mwambie kuwa asiwe mchokozi Kwa wenzake na asiwaonee wenzake Kwa maana taarifa zikija kuwa kafanya hivyo utamuadhibu Kama vile utakavyowaadhibu watakaomuonea.

Watoto wanaonewa shuleni na wananyamaza Kwa sababu Baadhi ya wazazi mnawazingua.

Elewa kuwa Kisaikolojia kila mtoto yupo tofauti. Wapo mqjasiri, wapo waoga, wapo wenye nguvu wapo wadhaifu. Lazima ujue kudili na kumjua mtoto wako yupo kundi gani.

Usilazimishe mtoto awe jasiri wakati yeye ni muoga, utamharibu kisaikolojia na shule ataichukia.

Mfundishe ujasiri kidogo kidogo, sio suala la miezi sita au mwaka mmoja Bali ni ishu ya muda mrefu mtoto huweza ku-achieve kuwa jasiri.
 
Back
Top Bottom