Shule zote zina watu ambao huonea wengine iwe kwa matusi, vipigo, vitisho, uharibifu, ngono n.k.
Athari za huu uonevu ni mkubwa sana kwa anayeonewa, Wazazi hatukai na watoto na kujua nini kina waathiri au nani huwaonea.
Je, tufanyeje kuondokana na hii hali?
NB:. Binafsi nimemwambia mtoto, sitaki aje kachaniwa madaftari, au kanyanganywa kitu fulani, sitaki aje aseme amepigwa.
Akichaniwa daftari yeye naye achane. Akipigwa ampige aliyempiga
Na nimewaambia na walimu wake pia kuwa mi nishamfungulia wangu, akiguswa atawagusa wamgusao.