Mpaka sasa sijaona ishara zozote za JK kushindwa uchaguzi..Je kama kutolewa kifanyinye nini?Ajitokeze mtu ndani ya CCM au upinzani waungane kuwa na nguvu moja?
Je kwa wabunge na Madiwani tunahitaji viongozi wa wenye sifa gani?Bila kuzingatia Chama,Dini,kabila na nk?
Wananchi wetu wapate elimu gani na itawafikiaje ili waweze kuchagua viongozi wanao wafaa?
Wadau wa JF watawezaje kuwa part na changamoto katika kueneza elimu hio kwa waTanzania wengi ili kuweza kuepuka matatizo yanayo jirudia kila uchaguzi.
Litakuwa jambo la busara kama TUME YA UCHAGUZI ikishirikiana na Taasisi ya vyuo vikuu, wakifanya zoezi la pamoja kuhakiki vyeti vya elimu hasa ya vyuo vikuu kwa waombaji wote wanaogombea Ubunge na Urais. Itatupunguzia kero ya watu kugushi sifa za elimu wasizostahili kama inavyodhihilika hivi karibuni.. Hili zoezi pia liwahusu wale wanaogombea ubunge wa Afrika Mashariki.
hakikisha kura yako inaenda chama cha upinzani. period. nini cha zaidi ya hapo? pia piga kampeni against sisiemu kwa nguvu zako zote, kwa mtu yeyote utakayemkuta, popote pale. ila tuzuie fujo wazee, haina dili.
... kingine ni wanaJF wengi kujitokeza kugombea nafasi za ubunge na udiwani ..... ni rahisi zaidi ku-initiate change ukiwa ndani ya system kuliko ukiwa nje