Nini kikwazo cha wasanii Filamu Tanzania kutokwenda kimataifa?

Nini kikwazo cha wasanii Filamu Tanzania kutokwenda kimataifa?

Lino brother

Member
Joined
Oct 8, 2024
Posts
7
Reaction score
5
Wanafanya tamthilia na Filamu tunaziona ila tunaweza kuchangia mawazo yetu nini kikwazo kinachotukwamisha toa mchango wako ukiwa mdau wa Filamu Tanzania 🙏🏾
 
Siku wakiacha ujinga na kujinasbisha na CCM watafika mbali.Wayaache mawazo yao yawe huru,shule wasisahau na kila muda wajifunze dunia inavyojizungusha kwenye muhimili wake.Mola awaangazie InshaAllah!
 
Kuna ulazima gani kwenda kimataifa? Wao wanataka kwenda kimataifa?
 
Ulazima upo ili waweze kukua kiuchumi na Kuitangaza nchi kiujumla

Ni jukumu lao kutangaza nchi? Wewe katika sekta yako unaitangaza nchi?

Kukua kiuchumi, kwanini usiwaze uchumi wa nchi nzima kukua ili wasanii nao wanufaike badala ya kutegemea soko la nje? Unawajua wasanii wa China? Unadhani wanategemea kuangaliwa Africa kupata pesa?
 
Mmetaja sababu nyingi ila sababu kubwa kabisa ni tatu
1. Ubora hafifu wa filamu (poor production)
2. Uwezo mdogo wa waigizaji na wazalishaji.
3. Uandishi mbovu wa story na script.
 
Waigizaji wetu hawana elimu ya kile wanachokifanyia kazi.
Fikiria, watu wengi katika sekta zao wanachaguliwa kutokana na kile alichokisomea ila kwa wasanii hasa wa muziki na maigizo ni tofauti.
Waigizaji wengi wa nchi mbalimbali katika wasifu wao utaambiwa huyu fulani alisomea uigizaji katika chuo fulani, alianza sanaa ya maigizo jukwaani na kadha wa kadha hadi kufika hapo alipo.
Huku kwetu sasa, marehemu Steven Kanumba (Mungu amrehemu) na mwenzie Ray Kigosi walikuwa wakitafuta wadada waigizaji kulingana na ukubwa wa makalio yao, urembo na ukubwa wa majina yao katika jamii.
Katika waigizaji wote unaowajua, hakuna hata mmoja mwenye elimu ya kile akifanyacho.
Nilisikikiza mahojiano ya Fredirick Bundala na yule mtanzania aliyepata kuigiza filamu mpya ya Jackie Chan. Hakupata kwa bahati mbaya hiyo nafasi, kujua na kusomea kile alichoombea nafasi.
Kukiwa na waigizaji wazuri, ubovu wa camera na vitu vingine hatutoviona. Sote tulikuwa tunafatilia siri ya mtungi.
Utofauti wa Siri ya Mtungi na tamthilia nyingine ni mbingu na ardhi. Ama maigizo ya kaole kipindi kile na kile kinachotokea sasa hivi ni mambo tofauti.
Waigizaji wengi wa Siri ya mtungi nadhani walipitia chuo cha sanaa Bagamoyo, wa kaole wengi walikuwa wakifundishwa misingi japo kwa uchache na ndio maana kila mtu alifit kwenye uhusika wake.
 
Sasa kama master mind na kiongozi wao ndio huyo kibushuti stivu Nyerere unategemea nini?
 
tatizo kuu linaanza kwenye uwekezaji wa hizo filamu wenyewe, pamoja uwezo mdogo wa screep witers, direcotr and technical department nyengine.
filamu sio muziki kama unaweza kupiga kelele tu mambo ya kenda vizuri, zinahitaji utaalamu mkubwa na uwekezaji.
na kwa wanaonaza kua atck ma actors wakahisi kuwa wao ndio tatito ni kuthibitisha kuwa upeo wao kwenye hayo masuala ni mdogo sana
 
Back
Top Bottom