Waigizaji wetu hawana elimu ya kile wanachokifanyia kazi.
Fikiria, watu wengi katika sekta zao wanachaguliwa kutokana na kile alichokisomea ila kwa wasanii hasa wa muziki na maigizo ni tofauti.
Waigizaji wengi wa nchi mbalimbali katika wasifu wao utaambiwa huyu fulani alisomea uigizaji katika chuo fulani, alianza sanaa ya maigizo jukwaani na kadha wa kadha hadi kufika hapo alipo.
Huku kwetu sasa, marehemu Steven Kanumba (Mungu amrehemu) na mwenzie Ray Kigosi walikuwa wakitafuta wadada waigizaji kulingana na ukubwa wa makalio yao, urembo na ukubwa wa majina yao katika jamii.
Katika waigizaji wote unaowajua, hakuna hata mmoja mwenye elimu ya kile akifanyacho.
Nilisikikiza mahojiano ya Fredirick Bundala na yule mtanzania aliyepata kuigiza filamu mpya ya Jackie Chan. Hakupata kwa bahati mbaya hiyo nafasi, kujua na kusomea kile alichoombea nafasi.
Kukiwa na waigizaji wazuri, ubovu wa camera na vitu vingine hatutoviona. Sote tulikuwa tunafatilia siri ya mtungi.
Utofauti wa Siri ya Mtungi na tamthilia nyingine ni mbingu na ardhi. Ama maigizo ya kaole kipindi kile na kile kinachotokea sasa hivi ni mambo tofauti.
Waigizaji wengi wa Siri ya mtungi nadhani walipitia chuo cha sanaa Bagamoyo, wa kaole wengi walikuwa wakifundishwa misingi japo kwa uchache na ndio maana kila mtu alifit kwenye uhusika wake.