The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Imani za watu, huvunjika na kupotea baada ya kupatwa na mtihani wa mauti.
Hapo hata wapendwa, mashehk, mapadri, wachungaji hulia kwa huzuni ya kuondokewa na mpendwa wake.
Ni ngumu kukabiliana na tukio la kuondokewa au kufiwa, lakini je Mungu ana kusudi gani juu ya Kifo?.
Kwa kuwa kila mtu ana amini juu ya ukamilifu wa Mungu, kwa nini katika suala la kuishi kuwe na upungufu wa ukamilifu wa Mungu.
Kwa nini suala la mauti liwe ni lazima kiasi cha kuliweka kama kawaida ya yeyote Pasi kujali ni tegemeo au ni mtegemea.
Hayo ni miongoni mwa mswali niliyojiuliza na kumuuliza Mungu mwenyewe, sababu najua wengi huogopa kumuuliza Mungu maswali Kwa hoja.
Binafsi nimewahi kumwambia Mungu nitakuuliza maswali tata, na kama kukuuliza ni kosa naomba nipe majibu kisha niuwe, Nilipoanza kupata majibu nikagundua wanaofundisha kuhusu Mungu wapo tofauti na majibu halisi ya Mungu kwa kuwa wanahisia tu, Na ndiyo maana mpaka leo nipo na majibu napatiwa kirahisi mno, kiasi hata waliosomea teolojia hawapati majibu.
Majibu ninayopewa na Mungu hayana utata wala hayamuachi Mungu kuonekana asiyemkamilifu.
Kila jibu lina ukamilifu, na ndiyo maana hata siku moja sintomlaumu Mungu kwa ninayoyaona au kutokea katika maisha yangu na dunia hii.
Sababu mimi ndiye muhusika mkuu wa yote. Na niliyachagua ili kumdhibitishia Mungu kama naweza kuyashinda na kuchomokea upande wa pili salama kabisa.
Hata yanikute yapi siwezi kujiuwa, kwa kuwa niliyachagua ili niyavumilie.
Wewe unayesukwa sukwa na magonjwa, umasikini, na kila aina ya dhiki ikiwemo kupoteza wapendwa wako.
Amini Mungu mwenye uwezo wa kuyazuwia hayo, kayaacha yakukute ili, uonyeshe utukufu wake, kwa kuuavumilia, kuyashinda na kuyakabili, sababu ni sehemu ya mkataba wako.
Katika mahusiano ni hivyo pia, uwe na mwenza pasua kichwa, hutakiwi kumuacha.
Ipo hivi.
Kabla yeyote hajazaliwa huko alikotoka kuna mkataba kaingia na Mungu mwenyewe.
Hivyo siku za mkataba zinapoisha ni lazima hurudi tena mbele za Mungu na kutoa matokeo ya mkataba.
Kwa kusema kipi umefanya na kipi hukufanya.
Na huo mkataba ndiyo sababu kuu ya Mungu kutofuatilia au kuonekana na yeyote katika hii Dunia.
Sawa na askari kuingia mkataba wa kwenda kumtwanga Idi Amini wa Uganda, unachoulizwa ni je unaweza kwenda kumtwanga?.
Ukijibu ndiyo naweza basi serikali inakupa vifaa vya kukamilishia zowezi hilo.
Ukifia katika uwanja wa vita, unarudishwa kuzikwa kwenu, na ukishinda pia unarudishwa kupongezwa.
Hiyo aina maana kama serikali imemtuma Askari akafe huko, huwez kuiuliza serikali kwa nini umemuua askari.
Kwa mfano huo ni kuwa ukijaza mkataba wa kuletwa Duniani kuna jambo inatakiwa ulifanye hivyo usipofanya muda ukaisha unakufa na ukifanya na muda ukaisha unakufa pia.
Kwa hiyo kifo si adhabu toka kwa Mungu bali ni njia ya kila mmoja kuingilia upande wa pili wa ulimwengu.
Ukifuatilia kisa cha Yesu Kristo, alilia sana siku rafiki yake Lazaro alipokufa, lakini binafsi alishangilia sana kifo chake kiasi akawaambia waombolezaji wake.
Msinililie mimi bali jililieni ninyi na watoto wenu. Sababu alijua akifa ataendelea kuishi, na alifurahi zaidi sababu alichotakiwa kufanya katika mkataba wake alikifanya vyema.
Sasa wewe msomaji unajua mkataba wako unakutaka ufanye nini hapa duniani, au ulikuja kuzurura kisha ufe na kutuachia vilio tu.
Chunguzeni sana huu utaratibu mpya uliozuka una maana gani.
Yaani mtu akifa watu wanaweka muziki na kupamba msiba, wana maana gani na wametoa wapi huu utaratibu ambao hata makanisa yameubariki.
Ni waislamu tu ndiyo hawana mbwembwe hizi mpya.
Lengo la walioanzisha huo utaratibu wana maana ya kuwa Mtu akifa hatupaswi kuhuzunika sana, bali kushangilia sababu marehemu kamaliza mzunguko wa kuishi duniani na anaelekea mzunguko mwingine.
Ama arudishwe kuja kumaliza vipenge alivyokosea, arudi kuanza upya au aingie katika ufalme wa Mungu baada ya kufanya vizuri sana.
Ukiona maisha yako yamejaa mateso, naasumbuko kwa kila kitu fahamu hawamu iliyopita uliitumia vibaya hivyo unasahihishwa kwa kile ambacho ulikifanya vibaya.
Watu fulani huiita karma. na wengine huiita kufa na kuzaliwa upya. Moja ya visa vya kufa na kurudi kuzaliwa tena katika Biblia Linapatikana Marko 9:13 ambako Yesu anadhibitisha.
Kama nabii Eliya aliyetabiliwa kuja kwanza kabla yake, alikuwa amekuja kwa jina la Yohana mbatizaji.
Kwa mwenye biblia soma kuanzia mstari wa kwanza.
Kwa hiyo kufa na kuzaliwa upya lipo na hata kuingia mbinguni kuketi na Mungu kupo pia, kazi ni moja kutekeleza mkataba wako hapa duniani.
Faida za kutekeleza mkataba zipo nyingi, moja kuu ni Mungu kukulinda ili ufanikishe, hivyo hata mtu akikusudia kukuuwa hawezi.
Kikubwa uwe kwenye harakati, ila ukiishi nje na mkataba ata mate yatakupalia ufe mapema sababu, huna faida.
Jiulize kwa nini katika ajali wanaweza kufa watu wote akatoka mmoja ni mzima kabisa.
Pengine mwenzio anajua nini anatakiwa kukifanya na yupo ndani ya mkataba, Mungu anamuondoaje mapema.