Nini kilikufanya ugundue Umri umeenda?

Ha ha ha niliingia ofisi ya Tanesco wamama ofisi nzima wananiamkia huku wakiwasihi wafanyakazi wengine 'HEBU MSIKILIZENI BABA ANA SHIDA GANI' Yaani mimi nawaona pisi kali wao wananiona baba duh!
😀😀😀Unajiuliza wananiambia mimi au kuna mtu nyumayangu au
 
Pale mama ambapo alinipigia simu, hakuniomba hela ila alinambia....
Emily magnus yaani sina hata chumvi ngoja nikakope....

Nikajua....
 
Siku nyingine nimemsindikiza Rafk angu kutafuta shule ya watoto, Mwalimu wa Taaluma akawa anatukaribisha pale ety "Karibuni ofisini Wazazi " Nikapata shock kua kumbe naonekana kama mzazi 😀
 
Siku nyingine nimemsindikiza Rafk angu kutafuta shule ya watoto, Mwalimu wa Taaluma akawa anatukaribisha pale ety "Karibuni ofisini Wazazi " Nikapata shock kua kumbe naonekana kama mzazi 😀
Hahaha ko kuitwa tu mzazi ukaogopa? Kuna wale wanaozaa wakiwa na umri mdogo probably 17 yrs, ko hao wakiitwa wazazi watakuwa wamezeeka
 
Ukishafika 35+ jua kabisa maji kupwa ,maji ya jioni ,jua linazama.
 
Hahaha ko kuitwa tu mzazi ukaogopa? Kuna wale wanaozaa wakiwa na umri mdogo probably 17 yrs, ko hao wakiitwa wazazi watakuwa wamezeeka

Kwa sasa kuitwa Mzazi Ni jambo zito kwangu, Kuleta kiumbe Duniani sio Jambo la mchezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…