SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Juzi wakati watu wanajadiliana ripoti ya mapato na makato ya mechi ya Simba na Yanga, kuna uzi nilitoa comment nikasema ile ripoti imeletwa maksudi kuiathiri Simba. Kuna mtu akanijibu kitu nikamwambia, asubiri mahudhurio ya mechi na Wydad.
Mechi ya jana ya Simba na Wydad ilikuwa na mahudhurio hafifu ukizingatia kuwa ilikuwa sikukuu, Simba ametoka kumfunga Yanga na pia umuhimu wa mechi yenyewe. Najaribu kutafakati nini kimesababisha hilo au ni muunganiko wa sababu mbalimbali na si moja.
Katika kuangalia mechi nyingine za robo fainali za CAFCL, mechi ya Simba ni kama ndiyo ilikuwa na mahudhurio madogo kuliko zote na hili ni jambo la kushangaza maana Simba imekuwa inasifika kwa mahudhurio makubwa katika mechi za CAF.
Ipi kati ya hizi unadhani ni sababu kuu?

- Hali ya hewa ya mvua
- Uchumi mgumu (na mahitaji ya sikukuu)
- Wasiwasi wa kupata matokeo mabaya
- Ripoti ya mapato na makato ya mechi ya Simba na Yanga
- Mfululizo wa mechi za hivi karibuni (mashabiki wamenunua sana tiketi)
- Uchaguzi wa Mgeni Rasmi
- Sababu nyinginezo (zitaje)