Joseph Kasela Bantu alikuwa ni mkuu wa mkoa wa kati ya Tabora au Shinyanga enzi hizo za Mzee Nyerere miaka ya sabini, siku moja aliitisha mkutano wa hazara, moja ya aliyozungumza katika mkutano huo ilikuwa kuhusu wezi wa mifigo na hasa ng`ombe. Alitaja kama kitu kuwasaka hao wezi wa mifugo ambao ilikuwa ni kero kweli kwa wasukuma.
Sasa inasemekana wasukuma na wanyamwezi walimnukuu vibaya huyo mkuu ukitilia maanani kabila hilo walikuwa mbumbu sana enzi na wengi walikuwa ni wapagani.
Baada tu ya mkutano wakatoka na silaha wakaanza kuwauwa hao wezi wa mifigo, wakawauwa wengi kama arobaini hivi, Mzee Nyerere kuuliza wakasema wamaamrishwa na Mkuu wa mkoa Kasela bantu wafanye hivyo. Nyerere alichofanya ni kumtia kizuizini mkuu huyo na ikawa ndiyo mwisho wake.