Nini kimefichika kuhusu jina Tanganyika?

Nini kimefichika kuhusu jina Tanganyika?

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Zipo siri nyingi zimefichika katika nchi hii na hakuna anayethubutu kuzisema hadharani kwa kujiamini pengine kwa sababu hazikidhi vigezo vya kisayansi lakini zinaathiri sana baadhi ya maamuzi ya kisiasa yanayoligharimu taifa.Mifano michache ni kama;
-Kuanzishwa kwa mbio za mwenge ambako kunahusianishwa na mkuu wa wachawi maarufu kama Forojo Ganze na Tambiko lililofanywa Lindi kuikabidhi Tanzania kwa Wachawi?(chanzo jf jukwaa la Historia) Na kwa hiyo kurudi kwa Tanganyika inaonekana kama ni kujitoa katika laana ya tambiko hilo?!!!Jambo ambalo ccm hawataki litokee?

-Mabishano ya kurejeshwa kwa Tanganyika yanayotokea leo na yaliyowahi kutokea hapo nyuma.Je huenda ni kwa sababu ya mabishano ya asili ya jina lenyewe ambapo baadhi wanahusisha na ziwa Tanganyika ambako inasemwa kwamba JK Nyerere aliisusia Kigoma kutokana na imani za kishirikina?!!!(Sijui walimfanyia nini hawa jamaa)

Je ccm huenda mmelishwa ngonjera zenu kutetea muundo wa serikali mbili ili mlinde viapo vyenu kwa shetani mliyemkabidhi nchi ya Tanzania(watanzania wawe mazoba) na mna hofu Tanganyika ikirudi mtadaiwa kurudi tena kuikabidhi Tanganyika kwa gharama ya damu za watu?!!(Kwani mnajua jinsi umbulula wa watanzania mnavyofaidika nao)

Natamani kujua yaliyo nyuma ya Muungano huu tata!Maana kama ni wizi wanaweza tu kuendelea kuiba hata kama Tanganyika ikirudi na vilevile wataendelea kuuza tu rasilimali zetu kwa wazungu,waarabu na wahindi kwa sababu wametudharau.Hili suala la serikali 2 wanalikomalia vile vile kama walivyokomalia suala la mwenge!Hawana hoja yoyote ya msingi zaidi ya propaganda tu.Nini siri ya kuikataa Tanganyika?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mwenge unahusiana moja kwa moja na ushirikina,Ndio maana watu wako kimya kuhusu muungano.Ndio maana tunaendelea kulishwa moshi wa mwenge tuendelee kuwa mtaji kwa ccm
 
Mwenge unahusiana moja kwa moja na ushirikina,Ndio maana watu wako kimya kuhusu muungano.Ndio maana tunaendelea kulishwa moshi wa mwenge tuendelee kuwa mtaji kwa ccm
Mwenge ndio tambiko. Na hili hata rais analijua kabisa. Siku mwenge ukizimwa vitu vingi vutafichuka
 
Mbona nilisikia mwenge wa mwanzo uliibwa tukaletewa mpya wa kutoka china? Kiwanda cha nchi gani kilitengeneza mwenge original? Ni nani alitoa wazo la kuzungusha mwenge? Au hawa CCM wanasubiri mpaka walioanzisha haya mambo wafe wote ili waendelee kutulaghai?

Tuanzie kuelimishana kuhusu hii idea nzima ya mwenge. Ninaamini wapo watu waliokuwepo na kushuhudia process nzima wakati haya mambo yanaanzishwa, mfano mzee Mwinyi na wengine, wapelekwe TBC wahojiwe hata kwa mtutu wa bunduki waseme tu kila kitu kiwe kwenye "permanent national archive". Tuige mambo mazuri ya wazungu, wao kila kitu kinahifadhiwa kwa ukamilifu na muda maalum ukifika kinawekwa wazi kwa vizazi vinavyofuata kujielimisha mambo yalivyokuwa.

Tusiendelee kutupiana lawama zisizokuwa na ukomo kila siku.
 
Back
Top Bottom