Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leo hata kwenye taarifa ya habari sijaona habari ya Dr kule Kyela, hajaenda na waandishi au?
Watu wa kanda hizo tunaomba habari!
Kulikuwa na watu wengi sana na hasa vijana. Dr. Slaa alionekana kama anampigia kampeni Dr. Mwakyembe badala ya mgombea wao.
Vijana wengi walikuwa wanasema kura ya ubunge Mwakyembe lakini urais Dr. Slaa. Kundi kubwa la vijana ni lile linalomwunga mkono Mwakyembe na ambalo lilimpa ushindi kwenye kura za maoni.
Wazee na akina mama walikuwa wachache. Kafanya mikutano Matema, Ipinda na Kyela mjini. Sikuhudhuria mikutano ya Matema na Ipinda kwahiyo sijui ilikuwaje.
Watu walikuwa wengi sana kuliko ule mkutano wa JK. Ila wana CCM ambao mimi nawafahamu walikuwepo wengi, haijulikani kama wanataka kumpigia kura Dr. Slaa au walienda kusikiliza tu mkutano wake.
Kama hawa vijana wote wamejiandikisha, basi Dr. Slaa anaweza kuwa na kura zake nyingi kuliko nilivyokuwa nafikiria mwanzoni ingawaje bado JK ana nafasi ya kuongoza kwa Kyela kwasababu ya kura za wanawake na wazee na pia mtandao wa CCM ambao uko kila sehemu. CHADEMA hawana uongozi wa kuhakikisha hawa wafuasi wao wanafuatiliwa na kuhakikisha wanapiga kura. Kikubwa hawana watu ambao wako tayari kufa wakilinda kura zao. Washabiki wao wengi ni wale wale CCM ambao wakirubuniwa kidogo wanaweza kurudi CCM.