Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Kipindi cha sakata la Membe,Makamba na Mzee Kinana kuhojiwa na kamati kuu Mh Membe pekee ndiye aliyegoma kuomba radhi kwa chama na viongozi kwa madai kuwa hakuna kosa alilofanya na alisema yuko radhi kufukuzwa lakini kamwe hatoomba msamha!
Na kweli Membe alifukuzwa chamani na kukimbilia ACT Wazalendo!
Jana wakati shaka anatangaza mabadiliko ndani ya Chama cha Mapinduzi alikaririwa akisema kuwa Membe na mwenzie Diwani wamekuwa wakiomba msamaha kwa chama na wakijutia makosa yao kwa muda mrefu na wameandika barua za kuomba radhi zaidi ya mara tatu hivyo baada ya kuomba sana msamaha chama kimeona kiwape msamha.
Bado najiuliza ni kweli Membe huyu aliyesema kuwa hana kosa lolote na hatoweza kuomba msamha kamwe kweli ameomba msamha na kama ameomba msamaha kumbe alikosea? Nini kimeyumbisha msimamo wake?