Nini kimemkuta Bernard Membe hadi kubadili msimamo wake mpaka kuomba msamaha mara tatu?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Kipindi cha sakata la Membe,Makamba na Mzee Kinana kuhojiwa na kamati kuu Mh Membe pekee ndiye aliyegoma kuomba radhi kwa chama na viongozi kwa madai kuwa hakuna kosa alilofanya na alisema yuko radhi kufukuzwa lakini kamwe hatoomba msamha!

Na kweli Membe alifukuzwa chamani na kukimbilia ACT Wazalendo!

Jana wakati shaka anatangaza mabadiliko ndani ya Chama cha Mapinduzi alikaririwa akisema kuwa Membe na mwenzie Diwani wamekuwa wakiomba msamaha kwa chama na wakijutia makosa yao kwa muda mrefu na wameandika barua za kuomba radhi zaidi ya mara tatu hivyo baada ya kuomba sana msamaha chama kimeona kiwape msamha.

Bado najiuliza ni kweli Membe huyu aliyesema kuwa hana kosa lolote na hatoweza kuomba msamha kamwe kweli ameomba msamha na kama ameomba msamaha kumbe alikosea? Nini kimeyumbisha msimamo wake?
 
Hata ungekua wewe, ungefanyaje?
 
Akihojiwa na ITV huyu Mwamba aliwahi kuulizwa kama atarudi CCM akakataa kabisa akisema Yeye ni kama Zitto au Maalim Seif ambao walifukuzwa kwny vyama vyao hivyo asilani hawezi kurudi.

Mwana siasa wa kumuamini ni yule aliezikwa tayari.
 
Kwani Membe sio Mtanzania? Maana Mtanzania kula matapishi Yale ni kawaida Sana.
 
Alishauriwa na Kikwete aombe radhi. Si unajuwa katika serikali hii JK ndiyo kila kitu, Mama yeye anakaimu tu ila kila kitu kinafanywa na Kikwete chini ya carpet na ndiyo maana unaona wale viongozi wote useless wanarudishwa tena madarakani.
 
Inawezekana msamaha alioomba ni wa kuhamia ACT Wazalendo tu
 
Akihojiwa na ITV huyu Mwamba aliwahi kuulizwa kama atarudi CCM akakataa kabisa akisema Yeye ni kama Zitto au Maalim Seif ambao walifukuzwa kwny vyama vyao hivyo asilani hawezi kurudi

Mwana siasa wa kumuamini ni yule aliezikwa tayari
Dah umenikumbusha aisee
 
Kwanza nikushauri asilan abadan usi wamini mwanasiasa. Kwanza siqmini kama membe aliwahi hama CCM ile yote ni propaganda, ile kwao ni kazi kumbuka walisha kula kiapo cha uaminifu utaumiza kichwa bure. Have a nice day
 
Wewe unaamini ameomba msamaha kweli?🤣🤣🤣

Hata kama ameomba kurudi kweli, hujui sababu ni nini? CCM ile na CCM hii zinafanana?

hawa wanaoshikilia chama kwa sasa wamemkaribisha, sababu walikuwa wakimuunga mkono chini kwa chini kipindi kile
 
Huyo Membe ni mtu wao wanaweza kumpamba vyovyote watakavyo ilimradi wamrudishe jikoni waendelee kula nae zabibu za taifa, usiamini hiyo sababu aliyotoa.
 
Hajaomba msamaha wowote. Aliomba lini? Ilibidi aseme hivyo maana mwandishi aliuliza. Kama unakumbuka vizuri kulikuwa na kutoelewana kuhusu kufukwa kwa Membe CCM nasikia man'gula alipinga. Kilichomkuta nadhani unakumbuka. Sasa wale waliopinga wamemrejesha maana hawakukubaliana na hoja ya kumfukuza.
 
Bado najiuliza ni kweli Membe huyu aliyesema kuwa hana kosa lolote na hatoweza kuomba msamha kamwe kweli ameomba msamha na kama ameomba msamaha kumbe alikosea? Nini kimeyumbisha msimamo wake?
Mkuu Leak , hili ni swali very valid, kwasababu wakati niliandika my psychoanalysis ya waomba msamaha Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity, kumhusu Membe nilisema
Hivyo naungana na wewe kujiuliza kulikoni?, ilikuwaje?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…