Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mkazi mmoja wa maeneo ya kati ya Israel amekamatwa na kikosi cha kijasusi cha Shin Bet kutokana na kutoa vitisho vya kutaka kumuua waziri mkuu wa Israel.
Wiki iliyopita kitisho kama hicho kilitolewa kwa waziri wa wa mambo ya usalama wa taifa,,Itamar Ben-Gvir ambaye ni mmoja wa mawaziri wenye kutoa matamshi makali daima kwa wapalestina ikiwemo matumizi ya bomu la nyuklia.
Hayo yakidhihirika waziri mkuu huyo tangu afanyiwe upasuaji wa ngiri siku chache zilizopita hajasikika akitoa yale matambo yake dhidi ya Hamas.
Operesheni hiyo ilifanyika kwa mafanikio ambapo mara alipozinduka aliweza kuongea na raisi Biden kuhusiana na mikakati yake ya kivita na kujibu lile karipio la rais huyo wa Marekani juu ya kupeleka jeshi la ardhini eneo la Rafah.
Netanyahu vie vile hajasikika (sijamsikia) akizungumzia kwa undani juu ya kupunguzwa kwa askari wake kutoka eneo lote la Gaza.
Kikawaida wagonjwa wanapofanyiwa upasuaji mkubwa hutakuwa kupata mapumziko na wajizuie kusema sana.
Katika siku za karibuni maandamano ya kumpinga waziri mkuu huyo na sera zake za vita dhidi ya Hamasa yamekuwa makubwa sana na kuongezeka kila uchao.
Muandamanaji mmoja alisikika akitoa maneno ya kudharau operesheni nzima ya Gaza akisema kwamba waliahidiwa kurudishiwa mateka wao lakini kinachotokea kila siku wanatuletea maiti za mateka hao.