Nini kimetushinda kuunganisha reli ya kati kutoka Kigoma hadi Burundi na Rwanda?

Kukarabati tuliyonayo tumeshindwa sembuse kujenga mpya??Hii iliyopo ikipita utadhani kali la kifusi limepita jinsi inavyotimua vumbi!!!
 
Walio kwenye nafasi za maamuzi ndio wamiliki wa magari ya kubeba mizigo.
Tukifufua reli Riz one atakula mawe?
Bujibuji mawazo hayo anawaza mtu, viongozi na chama imara siyo kiongozi DHAIFU NA Chama DHAIFU kama CCM.Maendeleo makubwa ni kugawa neti za mbu ambayo moja ni sh 2,500 sawa na apakati moja ya juice ya azam
 
Last edited by a moderator:
Hivi tumeshindwa nini kuunganisha reli ile ya kati toka kigoma hadi burundi na Rwanda? kufufua reli ile toka Tanga hadi Arusha to kenya? Moshi arusha mwanza? tatizo letu ni nini?

Afadhali mkoloni siyo tusi, walijenga sisi tulibomoa.
 
Ukijenga au kuimarisha reli malori ya mwana wa mkubwa yatafanya kazi gani?
 
Ufisadi tu umetujaa watanzania kwenye fikra zetu. Kama ingekuwa tunakaa chini na kufikiria wajukuu na viotukuu vyetu basi tungefika mbali sana. Wenzetu wanajali wajukuu zao ndio maana plan zao za miaka 200 ijayo.
 
serikali ya ccm ni sikivu. tumeshaliweka kwenye sera za ccm. tutalitekeleza hilo swala. hayo ndo majibu utakayo pewa ukimuuliza kiongozi yoyote wa serikali ya ccm. mia
 
Kwa viongozi gani tuliokuwa nao? Unakuwa kama mgeni wa hii nchi bwana hebu acha kututia hasira huko
 
Kukarabati tuliyonayo tumeshindwa sembuse kujenga mpya??Hii iliyopo ikipita utadhani kali la kifusi limepita jinsi inavyotimua vumbi!!!

Nimekutana na mtu anayejiamini katika kudai kwamba Wachina tayari wanafanya survey ya reli mpya ambayo itaanzia kwenye Bandari mpya ya Kikwete (Bagamoyo) na itakwenda parallel na reli ya Kati na hiyo ndiyo itakuwa na matawi ya kwenda Kigali (Rwanda) na Msimbati (Burundi). Anasema ujenzi wa reli hiyo na Bandari ya Kikwete lazima uanze kabla ya mwisho wa utawala wa Kikwete. Naomba mwenye habari zaidi atujuze.
 
Mimi naweza kulisimamia hili,mimi mwenyewe nlikua nmeajiliwa na kampuni moja ya wakenya kazi ilokua inafanyka ni kuangalia sehem reli itakapo pita,reli itatoka isaka shinyanga mpaka ngara.hapa ndo kutakua na matawi,kwa rwanda itapita rusumo na kwa burundi itapita rulenge mpaka kwnye mgodi wa nickel panaitwa bugarama mpka burundi,huu mradi uko chni ya bank ya dunia.
 
Ufisadi tu umetujaa watanzania kwenye fikra zetu. Kama ingekuwa tunakaa chini na kufikiria wajukuu na viotukuu vyetu basi tungefika mbali sana. Wenzetu wanajali wajukuu zao ndio maana plan zao za miaka 200 ijayo.


Tuache speculations, hii project ilishaanza na inaendelea. Wengi wetu huamini tunapoona ujenzi ukiendelea lakini kabla ya kufika huko kuna hatua za awali za Survey and Engineering design.

Source: AfDB
 
Baada ya Rais Kagame kutaka kupata huduma za Reli kutoka Uganda na Kenya, basi hiuu Mradi nafikiri umekufa kifo cha mende.
 
Wabongo sisi zetu longolongo tu hamnaga kitu.

Hizi stori za Reli hizi za miaka kibao but nothing is being done.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…