DOKEZO Nini kinaendelea barabara Tungi Morogoro? Pesa za fidia zimeliwa au iliamuliwa barabara ipishe nyumba zilizotakiwa kubomolewa?

DOKEZO Nini kinaendelea barabara Tungi Morogoro? Pesa za fidia zimeliwa au iliamuliwa barabara ipishe nyumba zilizotakiwa kubomolewa?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Morogoro Mjini kata Tungi (ambako ndio makao makuu NIDA mkoa) kuna ujenzi wa barabara ya lami, ni pongezi japo ujenzi ulicheleweshwa kwasababu za kisiasa kwani baadhi ya viongozi walikuwa wakisema fedha ya WORLD BANK ilishatengwa kwa barabara hiyo lakini imeenda kujenga barabara nyingine kata ya Kichangani kwa kuwa diwani wa kata ya Tungi hakuwa CCM alikuwa CHADEMA hivyo adhabu kwa wakazi wa Tungi ilikuwa ni kutowapelekea barabara ya lami kwa kutomchagua mgombea wa CCM 2015.

Sasa ujenzi ukiwa unaendelea, katikati ya Tubuyu na Njiapanda mafisa karibu na makaburi yaliyoondolewa bado kuna kona kona kali. Katika mpango wa ramani inasemekana barabara ilitakiwa inyooke na nyumba kadhaa zilipwe na kupisha ujenzi wa barabara, cha kushangaza zimelipwa nyumba chache ambazo zimeshabomolewa na barabara inatengenezwa huku kukiwa na vijikona vingi kama vinjia vya uchochoroni au mitaani.

Sasa ni kweli Serikali imeshindwa kuwalipa watu, au pesa kuliwa, kama watu wanavyozungumza mitaani? Kwani kinachofanyika ni dhahiri kwamba sasa barabara inapisha nyumba za watu.

Hivi ni kweli wanafanya hivyo kwa kuwa wameshindwa kuwalipa? jambo ambalo miaka kadhaa mbele hapatakuwa na muonekano mzuri, japo kwa sasa wakazi wa tungi wanaitamani barabara ya lami, tusijenge tu ilimradi ujenzi ukamilike na Serikali mbeleni italazimika kuwalipa tena watu ili kufanya marekebisho.
 
Hapo itakuwa pesa zishaliwa na wenye kamba ndefu, cha msingi angalia usalama wa watoto wenu.
 
Back
Top Bottom