KERO Nini kinaendelea kati ya NHIF na hospital ya tiba healthcare -Upanga? Inadaiwa huduma kwa wenye kadi za NHIF zimeachwa kutolewa ghafla

KERO Nini kinaendelea kati ya NHIF na hospital ya tiba healthcare -Upanga? Inadaiwa huduma kwa wenye kadi za NHIF zimeachwa kutolewa ghafla

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
NI takribani wiki mbili sasa kituo cha Tiba Upanga hakitoi huduma za Bima ya afya kwa sababu zisizoeleweka. Wagonjwa tunafika na hatupewi huduma. Tukipiga NHIF 199 tunaambiwa twende vituo vingine, wakati mafaili yetu yapo pale.

Hakuna taarifa kutoka NHIF wala hapo kituoni juu ya nini kinaendelea. Juzi tu Agakhan nayo ilikuwa na mgogoro na NHIF! Kama kuna makosa wawelekeze ili wajirekebishe ama kama ni mambo ya bei wakae siti moja wazungumze.
 
La Aga Khan nawaunga mkono NHIF, watatukaushia mfuko.. NHIF wanahitaji kuimarisha mifumo yao kupunguza ubadhirifu badala kuzuia hospitali..
 
Ila huo mfuko unaliwa na hizo hospitali binafsi, ugonjwa unaogharimu 70000 kwa wenye bima wataandika laki 3-4,
 
Hospital nyingi kwasasa ni kama hiyo huduma wanainyanyapaa. Hata Muhimbili kwenyewe naona huduma nyingi wameziondoa kwenye mfumo wa bima. Mfano. Wanakupasua halafu unaambiwa mpira wa kulishia puani, mgonjwa ananunua kwa cash, mpira wa kutolea mkojo catheter unalipia cash nk nk.. ... Si ni kama hakuna sababu ya kukatwa yetu sasa
 
Lipa cash kiongozi upone!! Wao unao washitakia hawatibiwi Tanganyika. Ni nje ya nchi tu
 
Hospital nyingi kwasasa ni kama hiyo huduma wanainyanyapaa. Hata Muhimbili kwenyewe naona huduma nyingi wameziondoa kwenye mfumo wa bima. Mfano. Wanakupasua halafu unaambiwa mpira wa kulishia puani, mgonjwa ananunua kwa cash, mpira wa kutolea mkojo catheter unalipia cash nk nk.. ... Si ni kama hakuna sababu ya kukatwa yetu sasa
We ndo umeongea pumba mwishoni japo ulianza vzuri.

Tusikatwe hela tutaweza kuwatibu wazazi wetu wenye dialysis na cancel??

Au unaongea sababu hayajakukuta
 
Back
Top Bottom