Mimi binafsi nikiangalia katika hivyo vyote naona kwamba hali ya uchumi ni nzuri na kama taifa tunaelekea sehemu nzuri.Kufungwa kwa biashara, watu kupoteza au kukosa ajira na biashara kuwa ngumu ni kawaida katika uchumi wa soko ambapo kuna ushindani mkali. Kama biashara imashindwa ushindani basi huwezi kusema ni matatizo ya serikali hapana ila iwapo maamuzi ya serikali ama kisheria au kisera ndo yamefanya biashara hio kuanguka basi unaweza kulaumu serikali na ni lazima kuwa makini katika kutoa lawama hizo kwani kuna uwezkano kabisa kutoa lawana hizo kukawa na madhara zaidi ya kiuchumi.
Je, baada ya kufanya oberservation yako ina maana uliona biashara zinafungwa kutokana na ushindani?!
Majuzi tu hapa tumeona taarifa ya bosi wa Tanga Cement akielezea ugumu wa biashara... je, sababu ya ugumu huo ni ushindani?! Fine, wapo watakaosema ni ushindani kutoka Dangote Cement lakini sio tu bosi huyo hakutaja Dangote Cement kama source ya ugumu wa biashara yao bali hata Dangote mwenyewe tunaona uzalishaji umepungua sana kiasi cha kufanya bei ya saruji kupaa!!!
Hapo kwa Dangote pia wapo watakaosema demand for cement ndio chanzo cha kupaa kwa bei licha ya kwamba nimesha-highlight suala la kupungua uzalishaji! Lakini pamoja na suala la kupungua uzalishaji, pia kuna taarifa nyingine inayohusu deni la karibu TZS 6 Billion ambalo Dangote Cement wanadaiwa na NSK Oil & Gas...
Dangote waliingia mkataba na hii kampuni ili iwe supplied with fuel. Ili NSK waweze ku-finance hiyo deal, wakachukua overdraft kwa Standard Chartered Bank!
Dangote kashindwa kulipa kiasi tajwa!
Kushindwa kwa Dangote kukaifanya NSK Oild & Gas ishindwe kuilipa Standard Chartered Bank!
Standard Chartered Bank nao katika kulinda pesa za wateja wake wakalazimika kwenda mahakamani kuishitaki Kampuni ya Mafuta! Kampuni ya Mafuta nayo ikalazimika kwenda mahakaman kuomba Dangote Cement ifilisiwe!!
Huo mfano wa juu ndivyo ulivyo kwa biashara nyingi!! Nani angetarajia Dangote washindwe kulipa 5.8B hadi wanafikishwa mahakamani?! Ukweli ni kwamba, biashara ni ngumu na ugumu huo hautokani na ushindani!!!
Ushindani pekee unaoweza kuiathiri Dangote Cement ni from imported cements, na kama ndivyo bado wa kulaumiwa hapo ni serikali kwa sababu huwezi kuacha viwanda vya ndani vinakufa kutokana na ushindani wa imported products wakati imported products zenyewe badala ya kurahisisha maisha, ndo kwanza zinafanya maisha yawe magumu kwa wajenzi!!
Aidha, kuna habari imesambaa hivi majuzi... ki ukweli nilishindwa kabisa ku-comment chochote manake hadi sasa nashindwa kuamini kama nilichoona mitandaoni ni kweli! Na hii ndo comment yangu ya kwanza kuhusu hilo suala... ni about Ngurdoto Mountain Lodge!
Kama ni kweli, hivi hotel kama Ngurdoto ina feli feli vipi kibiashara kirahisi namna hiyo?! Anyway, nimesikia hapa na pale kuhusu sijui family conflicts and other blah blah!!
Je, kama Ngurdoto ingekuwa kwenye ile peak yake pangekuwepo na hizo family problems au wana-Familia walio mbali kidogo na biashara wanaliona lihoteli likuuuubwa lakini hakuna wanachopata na hivyo kuanza kushikana uchawi?!
Hata kama pangekuwa na hiyo migogoro, serikali inafanya nini kuhakikisha miradi mkakati kama huu haitumbukii shimoni kwa mambo ya kijinga?!
In short, kosa kubwa kabisa alilofanya Magu ni kujikita zaidi kwenye Uchumi wa Kodi! Hajali kuona kampuni yoyote ile inakufa katika kuhakikisha kampuni husika inatoa hadi senti yake ya mwisho na kulipa kodi!!
Wakati anafanya haya anasahau kampuni husika ikishakufa, atapoteza PAYE pamoja na salary and wages itakayozunguka kwenye uchumi na ku-stimulate sekta zingine za kiuchumi, na hivyo kuleta kodi zingine zaidi na zaidi!!!
JPM na serikali yake HAWAJALI multiplier effect ya kiuchumi, no wonder wamewekeza matrilioni kwenye ndege!! Matokeo yake, baada ya kutengeneza mipango maalumu kuhakikisha kampuni zinazodaiwa kodi zilipe kwa awamu ili kuhakikisha zinaendelea kufanya biashara na hatimae ku-enjoy multplier effect, JPM na Serikali yake wao "kodi yetu kwanza", ukifa, it's up to you!!!
Unaachaje hotel yenye vyumba 300 na 7 Presidential Suites inageuka kuwa hostel ya wanafunzi (kama kweli)?! Serikali ya JPM kama ingekuwa inajali kama inavyotaka ionekane, ingeweza hata kununua kiasi cha shares za Ngurdoto na kufanya management contract kuhakikisha hotel inaendelea kufanya kazi huku ikiendelea kukusanya kodi zake!!
Kama nchi za wazetu, hususani US huwa wanafanya sana bailout kwa kampuni zao kwa vigezo walivyoweka wao, hata JPM angeweza kufanya bailout kwa kampuni zinazoelekea kuangamia hata kama kuangamia huko kumetokana na wao kutolipa kodi kwa sababu nchi maskini kama hii inatakiwa kuwa na goal kubwa ya kuhakikisha biashara nyingi zaidi zinaendelea kuzaliwa na zilizopo zinaendelea kukua!