Shin Lim
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 7,837
- 14,198
Habari wana jamvi na pia poleni na majukumu ya kila siku. Nimekuwa nikijiuliza swali hili mara nyingi na nikashindwa kupata majibu ya kujiridhisha kutoka kwa baadhi ya watu kutokana na majibu kuwa mepesi au ya kufikirika tu. Sasa leo naomba wenye uelewa mnisaidie tafadhali.
Hivi ni kwa nini kiungo/viungo vya upande wa kuume vina nguvu au uwezo zaidi kuliko vile vya upande wa kushoto?
1.Jicho: Jicho la kuume lina uwezo zaidi kuliko la kushoto. Uthibitisho upo kwa wapiga picha wakati wa kupiga picha hasa kwa camera za kizamani mara nyingi hutumia jicho la kuume.
2.Mkono: Watu wengi tunatumia mkono wa kuume katika shughuli zetu mfano kuandika, kula nk. Uthibitisho upo kwa karibu kila mtu.
3.Mguu: pia mguu imekuwa vivyo hivyo ila tu kuna baadhi ya watu huwa wana uwezo wa kutumia miguu yote hasa katika mchezo wa mpira wa miguu. Viungo ambavyo sijataja sina hakika kama na vyenyewe vipo kwa mtindo huo.
Watu wengi wamekuwa wakisema eti ni kwa sababu kuna tofauti ya idadi ya mbavu kati ya upande wa kulia na kushoto, wengine wanasema moyo upo upande wa kushoto ndio maana umeathiri viungo hivyo kutokuwa na uwezo sawa na vingine, sasa je huo moyo umeathiri mpaka macho?
Wapiga wanalijua hilo. Naombeni majibu tafadhali.