Nini kinafichwa kwenye mapinduzi ya Zanzibar?

mapinduzi ya zanzibar ni maandalizi yaloandaliwa nje ya zanzibar,okelo hana asili ya tanganyika wala zanzibar alijengewa historia ya uongo kuwa alikuwa anafanya kazi pemba kabla ya mapinduzi na hakuna mtu alewahi kumuona wala kuwa nae karibu ni mijitu ilizuka ikauwa wazanzibari na baada yakumali wakawapa vyama wapinzani madaraka ya serikali kwa wakati ule ambao ndio vilikuwa ASP hao kina karume na babu lakini karume alikuwa hana amri kwa vile serikali alipewa mikononi tu,mtazame okkelo alivyokuwa kwenye hio clip, yeye ndio alikuwa boss kubwa.

wao kina karume walijiingiza kwenye mapinduzi kwa kupata mteremko wa kuitwaa serikali ndio jambo walokuwa wanalipigania sana ni kushika madaraka ya serikali kwa hio waliingia kichwa kichwa na kujifanya na wao wameshiriki kwenye mapinduzi,mambo walokuwa hawayajui mwanzo wala mwisho wala hawakuyapanga, walovamia walijificha kwenye migongo ya vyama vya upinzani ili kupata uhalali wa kuua wazanzibari na kuondoa serikali ya waarabu ilokuwepo madarakani.

wakati huo kulikuwa na mfumo wa vyama vingi chama tawala cha warabu walikuwa wakijifanya wajanja kama vyama tawala vyote vinavyofanya leo, ujanja mkubwa walokuwa wakifanya ni kugawa majimbo sehemu ambazo walikuwa na watu wengi walikuwa wanakata majimbo mengi kwa kupata viti vingi na sehemu ambazo hawata watu majimbo yaklikuwa kidogo na viti vya uwakilishi vinapungua

sababu za uongo zilotumika ku-justify mavamizi(mapinduzi) yale ilikuwa ni waarabu wanawatesa waafrika huu ni uongo mtupu huyo mfalme wa zanzibar wakati ule alikuwa si muarabu safi alikuwa kama wazanzibari waliopo leo half cast,hizo zilikuwa ndio propaganda za siasa za wakati ule za kuwagawa watu kwa sababu waafrika walikuwa wengi kuliko waarabu kwa hio kupara wanachama wengi kwa siasa chafu ni kusema mnateswa na mpaka leo siasa hizo zinaendelea zanzibar ambapo ndio tuna serikali ya watu wetu waafrika ni ubaguzi mtupu,

mateso tunayopata wazanzibari saivi kwenye uhuru bandia mimi ningefurahi sana utawala wa serikali ya warabu ungekuwepo mpaka leo,kwa sababu wao walijitambua kama wazanzibari na sio wageni na walifanya maendeleo yote kwa ajili ya zanzibar yenyewe na sio nchi za waarabu. Zanzibar ingelikuwa sehemu kubwa sana kwa afrika nzima na kusingekuwa na ubaguzi wowote,mtazame babu katika hii video anavyoongea kiiengereza na alikuwa na elimu kubwa sana ambayo serikali ya zanzibar ndio walitoa elimu kwa watu wote bila ya kujali mweusi au mwarabu,wazanzibari wengi walikuwa wakiamini elimu ni ukiristo ndio hawakupata elimu. wazanzibari waarabu wengi wlikuwa hawajui kusoma na kuandika

leo tazama tulipo hatuna nchi,hatuna mali,hatuna umiliki wa chochote,chako ni chako mpaka wakikihitaji wanachukua kwa nguvu ndugu zetu hawa walioshika madaraka bila ya kujali kuwa wao na sisi ni kitu kimoja,tuna malengo mamoja
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Mkuu una hoja nzito sana.
 
Kumbe damu zilimwagika sana?
 
Mwinyi Mkuu ndio Sultan wa kwanza wa Zanzibar kabla ya kuja kwa Waarabu na alikua Mweusi, emu sema na sasa Mapinduzi yana faida na Muungano una faidi hili utalisikia kwa Zanzibar waliosoma na wakaishi pande zote mbili watakwambia Zanzibar inalindwa na Tanganyika na hio ndio ilikua Formula

Sababu historia inaongea waafrika hawakuishi Zanzibar baada ya Waarabu waafrika wamekua wanaishi Zanzibar zaidi ya miaka 30,000 iliyopita kabla ya ujio wa Waarabu, Wazungu na Warumi kwanini usijivunie cha kwako ukakijenga?
 
Ila historia ni ndefu, Wapemba wanakwambia chanzo cha Mapinduzi ni pale mwarabu alipokabidhi madaraka kamili kwa mpemba bwana Mohammed Shamte waunguja wakalianzisha vagi front akawekwa Okelo kutoka Uganda
Baada ya kusoma uzi huu nimepitia vyanzo kadhaa kuhusu Mapinduzi.

Nikiri kabisa kwa umri wangu huu nilikuwa sifahamu chochote kuhusu Mapinduzi ta Zanzibar.
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
Kwanini yaitwe matukufu, kuna utukufu gani hapo, katika umwagaji damu?
 
Haya ni mahojiano yaliyofanyika muda mfupi baada ya mapinduzi ya zanzibar.

Sikiliza mahojiano ya Karume, Babu na Okello ( mapinduzi ya zanzibar haya kuwahusisha wanasiasa )


Mohamed Said Pascal Mayalla
Wajomba wa samia walichinjwa kama mbuzi [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] nisiku za kupendeza sana siyo hawa waisiharamu tulio nao sasa wanao muabudu muarabu na wakristo wanao muabudu muisrael....hii ndiyo sababu samia anamchukia sana Karume na nyerere kuliko magufuli na kwa sasa samia yupobioni kumrudishia muarabu nyani wake.
 
Haya ni mahojiano yaliyofanyika muda mfupi baada ya mapinduzi ya zanzibar.

Sikiliza mahojiano ya Karume, Babu na Okello ( mapinduzi ya zanzibar haya kuwahusisha wanasiasa )


Mohamed Said Pascal Mayalla
Nimefurahishwa na majibu ya Okello. Mungu wa waafrika ndiye alikuwa nyuma ya nguvu aliyokuwa nayo. Naona, Ndugu zetu wa kaskazini (Ulaya) hawafurahishwi na Mungu Wetu wanafanya Kila Hila kutusahaulisha huyu Mungu. Tumeyaona Hata wakati wa COVID-19!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…