Nini kinasababisha albinism (ualbino)?

Nini kinasababisha albinism (ualbino)?

ENZO

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
4,244
Reaction score
1,741
Naomba kujua kinachosabaisha Ualbino kitaalamu zaidi, maana katika kuuliza uliza kila mtu amekua akinipa jibu lake, wengine wanasema ni kurithi, unakuta baba ni mweusi na mama ni mweusi lakini mtoto anakuwa na albinism.

Je, ualbinism unatoka kwa mama au kwa baba?

Tupige vita uuaji wa ndugu zetu wenye Albinism (Ualbino).
 
ni mambo ya GENETICS mkuu.ni kweli wanarithi toka kwa wazazi au mabibi na mababu huko.
Mtu anaweza akawa na GENE ya albinism lakini yeye asiwe albino, lakini akikutana na mtu mwingine ambaye naye ana GENE hiyo, hapo ndio mtoto anaweza kuzaliwa akiwa albino..
Ngozi ya binadamu ina matabaka(layers) mbalimbali. Kuna layer inaitwa MELANIN,hii ndio huipa ngozi rangi ya asili,na kuakisi mwanga wa jua hii husaidia mtu asipate kansa au matatizo ya ngozi kiurahisi. Sasa mtu akizaliwa bila hii layer,MELANIN, ndio anakuwa albino.
Hivyo suala la wazazi kuwa weusi na mtoto kuwa albino linawezekana kabisa..lakini pia mama anaweza kuwa albino na baba asiwe albino na wakapata mtoto asiye albino.....Is the matter of genetics.
 
nimalizie kwa kusema... kwa kawaida mtoto kuwa albino ni mchango wa wazazi wate wawili...sio baba tu au mama pekeyake...
 
ISLETS nimekuelewa mkuu, je mtu atajuaje ana hiyo GENE?!
 
Last edited by a moderator:
Naomba kujua kinachosabaisha Ualbino kitaalamu zaidi, maana katika kuuliza uliza kila mtu amekua akinipa jibu lake, wengine wanasema ni kurithi, unakuta baba ni mweusi na mama ni mweusi lakini mtoto anakuwa na albinism.

Je, ualbinism unatoka kwa mama au kwa baba?

Tupige vita uuaji wa ndugu zetu wenye Albinism (Ualbino).

Shahawa Nyepesi Zinazosababishwa Na Tabia Ya Wanaume Kupenda Kuwa Wanachama Wa ( CHAWAPUTA ) Ndiyo Sababu kubwa Ya Albinism.
 
Hiyo ni ukosefu/upungufu wa melanin ambayo ni inahusika na rangi ya ngozi

Kibaiologia inawezekana mmoja kati ya wazazi wa mtoto akawa heterozygous kwenye albinism hivyo kupelekea kupata mtoto ambaye ni homozygous Albino...hii ni genetic disorder ambayo inaweza kumkumba yeyote kwa kuwa hakuna kipimo cha moja kwa moja kujua kama kuna mwenye hilo tatizo wakati wapenzi wanapoambua kuzaa!
 
ISLETS nimekuelewa mkuu, je mtu atajuaje ana hiyo GENE?!

ENZO, kwanza tambua kuna aina kama 5 za albinism,japo zote zinahusisha hizo genes.
Ndio mtu anaweza kuchunguzwa DNA yake ili kujua uwepo wa genes zinazohusiana na hiyo kitu.. hivyo si kwa kuangalia tu kwa macho.
na pia kuna njia za kupima kujua kama mtoto atakiwa albino hata kabla hajaliwa(akiwa tumboni)..
 
hapo nimekusoma mkuu!' ............ mana nilishangaa sana kuona wazazi weusi halafu mtoto ana albinism! hiv haina dawa mtu akishajua ana hiyo GENE.
 
by dr.elina,, albinism intatokana na ukosefu wa pigment inayoitwa melanini ktk ngozi, na kwakweli tatizo hli linaweza kurithshwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto
 
hapo nimekusoma mkuu!' ............ mana nilishangaa sana kuona wazazi weusi halafu mtoto ana albinism! hiv haina dawa mtu akishajua ana hiyo GENE.

mkuu hakuna dawa ya kubadili hizo genes... mtu ukiwa nayo ndio basi tena..
 
mkuu hakuna dawa ya kubadili hizo genes... mtu ukiwa nayo ndio basi tena..

Na vipi kuhusu ulemavu mwingine?! kama wa viungo, pia ni Genes au?!
 
ya genes ni sababu moja wapo hasa genemutations, pia inawezekana ni upungufu wa madini fulani mwilini ndio maana mama mjamzito anashauriwa sana kutumia vyakula vyenye folic acid au hata supplements zake pale imapobidi na Iodine hii husaidia sana kuzuia ulemavu usio wa lazima.
pia pombe pombe na sigara sana huchangia hizi defects.
Kemikali na mionzi pia ni hatari kwa mtoto, hivyo vinaweza kuharibu chromosome abnormalities na mtoto akawa kilema. Hizo kemikali zinaweza zikawa hata ni haya madawa ya magonjwa, mama mjamzito kabla hajaanza kutumia dawa inabidi aonane kwanza na daktari ili amuhakikishie kama hiyo dawa haitamdhuru mtoto.

But point inabaki palepale kuwa cases nyingi hutokana na hizo genes kama matokeo ya chromosome abnormalities.
 
Back
Top Bottom