Naomba kujua kinachosabaisha Ualbino kitaalamu zaidi, maana katika kuuliza uliza kila mtu amekua akinipa jibu lake, wengine wanasema ni kurithi, unakuta baba ni mweusi na mama ni mweusi lakini mtoto anakuwa na albinism.
Je, ualbinism unatoka kwa mama au kwa baba?
Tupige vita uuaji wa ndugu zetu wenye Albinism (Ualbino).
ISLETS nimekuelewa mkuu, je mtu atajuaje ana hiyo GENE?!
ENZO, kwanza tambua kuna aina kama 5 za albinism,japo zote zinahusisha hizo genes.
Ndio mtu anaweza kuchunguzwa DNA yake ili kujua uwepo wa genes zinazohusiana na hiyo kitu.. hivyo si kwa kuangalia tu kwa macho.
na pia kuna njia za kupima kujua kama mtoto atakiwa albino hata kabla hajaliwa(akiwa tumboni)..
hapo nimekusoma mkuu!' ............ mana nilishangaa sana kuona wazazi weusi halafu mtoto ana albinism! hiv haina dawa mtu akishajua ana hiyo GENE.