Jamani wana JF mimi hili linaniumiza kichwa kila siku hivi kweli ni nini kinashindikana kwa serikali kuamua kuyauza magari yote ambayo yanaliingiza hasara taifa na kubakiza gari moja kila idara la aina hiyo kwa kazi maalum?
Wiki jana nilikuwa India, nikaenda chuo kikuu kimoja kaskazini mwa nchi, Nilicho kiona ni kuwa mkuu wa chuo anatumia gari aina ya toyota carina saloon. Chuo kina gari moja kubwa saizi ya landcruiser ambayo hutumika kama kuna haja ya kwenda labda NewDelhi au kwingineko mbali.
Ukiangalia maofisi yetu mengi ni aibu, chukulia vyuo vikuu vyetu kila mtu ni Landcruiser VX/GX au Nissani Patrol je kuna tatizo gani hapo?
Naombeni wanaJF tusaidiane kulieleza hili na wale ambao mko karibu na mh. kawambwa aulizwe ni nini kinashindikana? Mbona magufuli aliweza kurudisha gari zote katika himaya ya serikali na nakumbuka Prof. Mshana wa UDSM wakati akiwa CADO enzi hizo alishushwa kwenye land criuser lake na polisi pale ubungo na likaenda kubadilishwa namba, kawambwa anashindwa nini?
Naombeni mawazo yenu