baba yangu alikuwa ni mwalimu,alifariki 2004 na mirathi ilitoka mwaka 2005 kipindi hicho tulikuwa wadogo hatukuwa tunafaham sana kuhusu mirathi lakini aunt yetu ndo aliyekuwa msimamizi mama hakushirikishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ndugu zetu kuwa wababe sana,mirathi ilitoka na kugawanywa walivyopenda wao mama hakusema kitu wala kupinga alikaa kimya na kusema ni mambo ya kidunia yanapita tu acha wafanye wapendavyo.
tumekuwa kwa shida sana na mama yetu amekuwa msitari wa mbele kuhakikisha tunapata elimu kwani aliamini ndo mkombozi wetu.kipindi chote wakati tunaomba mikopo bodi ya mikopo elimu ya juu tulikuwa tunaomba death certificate ya baba na kuambulia kupewa copy tu na aunt ambaye ndie msimamizi wa mirathi ukimuuliza original anakuwa mkali hatoi majibu mazuri.
sasa mwaka huu mdogo wangu alikuwa anatuma maombi na mimi ndo nilikuwa namsaidia hivyo tukahitaji death certificate ya baba,nikampigia simu aunt akasema hana kama nina shida nacho niende mahakamani wakanipe nikamsihi sana akasema yeye alipewa pia copy original ilibaki mahakama ya mwanzo hawakumpa kumuuliza sababu za wao kukaa nacho ni nini hasemi ni mkali sana.basi nkamwambia anitafutie hata copy tu akadai nimpe pesa akakifuatilie nikampa akaja na copy sikusema kitu ingawa kwenye kucertify vyeti walitaka original nilipata shida sana kuwaelewesha.
siku moja mama kanipigia simu akaniambia aunt amemfuata na kumwambia kuna pesa ambayo mama mjane anatakiwa kupewa kila mwezi kwa ajili ya kujikimu na alitakiwa apewe toka baba alipofariki hivyo afanye madai ya miaka yote,pesa hiyo imeleta ugomvi mkubwa sana kwakuwa aunt anadai igawanywe na pesa yenyewe si nyingi kivile,nimemshuhudia mama yangu akipata shida miaka yote leo hicho kipesa kidogo ambacho ni haki yake kigawanywe tena hiyo ni haki kweli??.
kwa wenye uelewa je,nyuma ya hiyo death certificate ya baba yangu kuna nini kinaweza kuwa chanzo cha cheti hicho kubaki mahakamani?.
na je,mbali na mirathi na hiyo pesa ya mjane je,inawezekana kuna madai mengine yapo ambayo hatuyajui?
nilisikia watoto chini ya miaka 18 huwa wanapewa pia mafao je, ni kweli??.
nawasilisha kwenu wadau.