Nini kinaweza kuwa chanzo cha Kuku kuvimba macho?

anderson mbonika

Senior Member
Joined
Feb 28, 2017
Posts
112
Reaction score
56
Natumaini wote mko salama,

Kama heading unavyo jieleza na picha Kuku hawa waliuwa niwazima ila siku za hivi karibuni wameleanza kuvimba macho. Na kuhusu swala la chanjo wote wamesha pata.

Naomba ushauri wa Kitaalamu na wa kiuzoefu kwa wote ambao wamewahi kupatwa na changamoto kama hii

Naomba msaada ili niweze kuwaokoa hawa Kuku

Kuna dalili nyngne isokua uvimbe umeiona kwa hao kuku?
 
Dalili nyingine uliopo wakonna hope Hali ya kunyong'onyea
Kama kuna uvimbe yawezekana ikawa ni dalili ya infectious coryza ( mafua) angalia dalili nyngn km wanatoa maji maji ( mafua) au funua kope angalia kama kuna utando mweupe kama ni sahihi watafutie dawa ya mafua

Kuongezea hakikisha wanapata mboga za majani kama itakua ni upungufu vitamin A hivo watapona na wataongeza hamu ya kula na kuchangamka kama kawaida

Au unaweza kununua mchanganyiko wa Vitamin (Dukani) hasa zile zenye Kiwango kikubwa cha vitamini A

Pole mkuu kwa changamoto
 
Kuhusu dawa watakuelekeza wataalam,
Ila kama kuku wamezidiwa macho hayaoni kabisa,anza huduma ya kwanza hapo ndani kwa juu kuna utando mweupe ukikamua ngozi ya juu ya jicho unatoka,ukifanikiwa msafishe vzr kwa maji vuguvugu,wkt unasubiria dawa.
 
Mimi sio daktari.
Ila nakumbuka baba alikuwa anafuga broiler huo ugonjwa uliingia wale kuku waliambukizana,na macho wakishindwa kuona hata kula hawali.
Mwisho wa siku wanakufa.
Pale nyumbani palijaa makaburi ya kuku unaweza ukalia.
 
Antibiotics ztamsaidia atumie oxyvit (OTC +vitamin) .tuone mrejesho utakuaje
Kuhusu dawa watakuelekeza wataalam,
Ila kama kuku wamezidiwa macho hayaoni kabisa,anza huduma ya kwanza hapo ndani kwa juu kuna utando mweupe ukikamua ngozi ya juu ya jicho unatoka,ukifanikiwa msafishe vzr kwa maji vuguvugu,wkt unasubiria dawa.
 
Reactions: 1gb
Akutumia hata dawa mpaka wakaisha.
Mimi sio daktari.
Ila nakumbuka baba alikuwa anafuga broiler huo ugonjwa uliingia wale kuku waliambukizana,na macho wakishindwa kuona hata kula hawali.
Mwisho wa siku wanakufa.
Pale nyumbani palijaa makaburi ya kuku unaweza ukalia.
 
Bila kusahau fanya kuwaatenga wanaomwa na wale ambao bado ni wazima ili kuzuia maambukiz zaid
 
Mimi sio daktari.
Ila nakumbuka baba alikuwa anafuga broiler huo ugonjwa uliingia wale kuku waliambukizana,na macho wakishindwa kuona hata kula hawali.
Mwisho wa siku wanakufa.
Pale nyumbani palijaa makaburi ya kuku unaweza ukalia.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2960][emoji2960] nashukuru mkuu
 
iyo ni infectious coryza (mafua makali ya kuku) hii inasababishwa na bacteria ambao hutokana kutoweza kusafisha banda pia na kuku kukosa hewa bandani na vitu vingine vyo ugonjwa huo unaweza kutibu kwa dawa zifuatazo tylosin na fluban
 
Shukran mkuu
 
Ugonjwa wa ndui wakati fulani dalili zake zinaendana kabisa na ugonjwa wa mafua,utofauti ni kwamba ndui uvimbe huambatana na vidonda kichwani.Huyo kuku unadalili zote za mafua makali,tumia dawa walizoshauri wadau ila sishauri utumie fluban kwani uwezowake ni fafifu wakati huyo kuku amezidiwa tayari
 
Hao kuku wanaangalia sana TV.

natania.. ila pole sana huo ugonjwa ukiuzembea wataambukizana Banda zima..

Mie nilikuw nawaosha kwa maji ya chumvi yaan napasua ule uvimbe nasugua na maji ya chumvi.. wanapona
 
... yes, hata mie nna experience hiyo...watenge waliovimba macho, wasafishe kwa maji ya uvuguvugu yenye chumvi. Wape dawa wote wenye dalili na wasio nazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…