Nini kipimo cha Akili?

nyambaterito

Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
51
Reaction score
46
Nimejaribu kujiulizaa, hivi akili ya mtu huwa inapimwa na nini? Mpaka inafikia mtu anakuambia hauna akili wewe. Maana ukifeli mtihani unaambiwa huna akili je mtihani ndio kipimo cha akili, ukishindwa kufanya jambo fulani pia utaambiwa huna akili🤔, Kwanini?

Hapa kwa upande wangu nachofahamu kuwa kwa upande wa shule mwanafunzi huwa tuna mjaji kwa mitihani na hiyo bado hata kama akifeli sidhani kama itakuwa sawa kusema hana akili, bali atakuwa ameshindwa tu kufaulu kwenye hiyo mitihani maana kwa upande mwengine mtu hawezi kujua masomo yote atajua baadhi tu ya hayo sasa kama ameweza kufaulu kiingereza akashindwa kufaulu hesabu bado utasema hana akili.

Pia kuna mwengine kuhusu masomo hawezi ila kuna kitu ataweza kukifanya nje ya hayo masomo tena akafanya vizuri zaidi bado utasema hana akili? Pia tukija swala la utendaji kitu fulani au kazi fani, utakuta mtu hakufanya kwa uweledi mzuri bado ataonekana hana akili je nisa hihii kusema hana akili au hana uzoefu na uweledi na hilo?😥

So ni nini haswa kipimo cha akili na kwa nini tuseme mtu hana akili?🤔🙏 Ni mawazo yangu yanayoitaji msaada.
 
Akili hupimwa na changamoto mtu anazotatua na kama atatatua kwa weledi basi huyobana akili ila kama changamoto za maisha za mgalagaza kwa mda mrefu mtu huyo huchukuliwa kama fala au zoba

Akili hupimwa na changamoto mtu anazotatua na kama atatatua kwa weledi basi huyobana akili ila kama changamoto za maisha za mgalagaza kwa mda mrefu mtu huyo huchukuliwa kama fala au zoba

 
Kwa hyo usipo fanikiwa unakuwa huna akili?
 
Akili ni kile unachobaki nacho baada ya kuondowa vyote ulivyofundishwa shule, hiyo ndio akili.

Kuna mapumbavu yana mpaka masters na PhD lakini hayana akili.
😀😀 eti masters na PHD...umetisha@ Matola
 
Akili haina kipimo mkuu...kuna saa ipo... kuna saa haipo...kuna saa ni kubwa, kuna saa ni kidogo... yani akili ni kama hewa...
Nakubaliana na wewe mkuu.Lakini hapo inapokuwepo nini kinafanya tuseme unaakili na hapo isipokuwepo au inapokuwa kubwa ni nini kinasababisha haswa. Kwa mfano kwa upande wa darasani mtu akipata maksi nyingi ndo huwa tunamchukulia kuwa. ndo anaakili sana lakini mtu hyo ukimpeleka upande B hawezi kufanya kama darasani na kwa kile alichokishindwa basi watu watamwona hana akili.
 
Akili inapimwa kwa uwezo wako wa kutatua changamoto.

Mfano enzi zile la kituo cha mabasi ya mikoani kiko Ubungo, unakuta mtu ameachwa na basi la mkoa halafu anakodi pikipiki ya kulikimbiza gari. Pikipiki inalikimbiza basi mpaka Kibamba CCM au Kibaha ndo inalikuta. Gharama ya pikipiki unalipa zaidi ya tiketi ya hilo basi unalolikimbiza.

Na huyo ni mtu ambaye halali guest, yuko nyumbani kwake au kafikia kwa mtu.

Sasa si bora tu ungeahirisha safari uende kesho. Kuna mabasi hata penati hawakupigi, ila hata ukilipa penati inakuwa ni ndogo kuliko kulikimbiza basi kwa bodaboda.

Kuna watu walikuwa wanakimbiza eti hadi mabasi ya kwenda Tanga tu hapo... nauli Tshs. 15,000 halafu analipa bodaboda Tshs. 30,000 kulikimbiza basi.

Hao utasemaje.... wana akili?

Basi ndo akili hupimwa hivyo. Uwezo wako wa kubuni (kama hakuna) kutafuta (kama zipo) na kuchagua (ukishazipata) njia mbalimbali mbadala za kutatua changamoto.

Kuhusu mitihani ya darasani ndo maana maswali ya homework au ya mtihani kwa kiingereza huwa yanaitwa pia problems. Kwa hiyo na yenyewe ni kipimo kilekile tu cha uwezo wako wa kutatua problems.
 
Akili ni uwezo wa mtu kutenda na kufanya maamuzi kulingana na umri, mazingira, hali, mahali na uwezo halisi alionao huyo mtu.
Si kila jambo linalotumia akili lazima lifanikiwe. Kuna wakati utashindwa japo umetumia akili. Inategemea na vichocheo husika.

Kuna tofauti kati ya akili ya maarifa (knowledge) na akili ya elimu (education) Si kila mwenye kiwango kikubwa cha elimu ana akili kuzidi wasio na elimu. Japo wengi tunapima uwezo wa akili kwa kutumia level of education na sio knowledge.

Tunaheshimu mawazo ya proffesor hata kama hayako sahihi na kudharau mawazo ya asiyesoma hata kama yako sahihi.

Ila ukisoma historia za wavumbuzi wengi hawakuwa na elimu kubwa ya darsani bali walikuwa na maarifa yaliyowawezesha kupata ujuzi na kuutumia kusaidia kutatua changamoto
 
Umetisha mkuu.Lakini sasa utakuta huyo huyo aliyefukuzia boda boda kwa ajili ya basi lililomwacha tena kwa gharama zaidi hata ya hyo nauli kuna jambo huwenda alilifanya na akaonekana akili zipo.Hapo nachoona mimi basi sisi sote tunaakili lakini utofauti unakuja pale kama ulivyosema kutatua matatizo kwa uweledi hivyo basi kunawakati tutakuwa na akili na kunawakati hatutakuwa na akili si ndivyo?
 
Asante sana,Umenifunza kitu hapo kati ya akili na maarifa,basi itakuwa asilimia kubwa tunazo akili ila sasa maarifa ya kutumia hizo akili ndo hakuna.Umetisha✊
 
Hii nayo mada nyingine "NINI MAANA YA MAFANIKIO?"

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli. Kila mtu kuna maamuzi anayopatia na anayokosea. Yule ambaye anasemwa kuwa hana akili kiuhalisia ni yule mwenye matatizo makubwa ya kiakili kiasi kwamba hata yale mambo ya msingi kabisa anashindwa kuyafanya kwa kupatia.

Lakini kwa mambo mengine mengi kila mtu kuna anapopatia na anapokosea. Sasa unapokosea na kurudia tena na tena makosa yaleyale hapo ndo unaonekana huna akili. Unapokuwa unakoseakosea mambo mengi ndo unaonekana huna akili.

Kijamii kipimo kikubwa cha akili ni pesa na maneno yako. Ukifanya jambo kwa gharama kubwa kuliko kawaida unaonekana huna akili. Ukiwa na pesa unaonekana una akili. Ukiwa huna au ukizipoteza unaonekana mjinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…