Jibu ndio hilo. Uzuri sauti ya umma imesikika; CCM waipuuze kwa ujinga wao wenyewe. Hata ukichakachua matokeo huwezi kuchakachua dhamira ya wananchi ya kutoka kung'oa mfumo wa kifisadi na kujenga misingi ya taifa thabiti kiuchumi, kijamii na kisiasa. Slaa ameshaingia katika historia ya nchi hii kama mtu aliyeleta mageuzi ya kweli. Kuingia Ikulu si kigezo kikubwa kama hicho alichofanya. Mafisadi/Mamafia wanao uwezo wa kumweka yeyote hata asiye na uelewa au mpuuzi ndani ya Ikulu. Kumbuka Mobutu na Marekani. Sasa mapambano yaendelee viwanjani (bungeni + halmashauri) kwa kishindo zaidi ili waelewe wenye nchi yao wako macho masaa 24!