Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,039
- 5,560
Mimi sio mwana siasa ila nimewaza sana endapo hii kampeni Chadema walio kuja nayo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Chadema kuelekea uchaguzi mkuu wamekuja na kampeni ya NO REFORM NO ELECTION, kampeni hii inalenga mabadiliko katika tume kuu ya uchaguzi. Ikiwa na maana bila mabadiliko hakuna uchaguzi utakao fanyika, hii ni noma sana.
Katika kampeni ambazo Chadema wamewahi kuja nazo hapo kabla hii kampeni binafsi nimeielewa na kuikubali. Chadema wanataka mabadiliko katika tume kuu ya uchaguzi, mabadiliko yatakayo fanya uchaguzi uwe wa huru na haki. Kwa mantiki hiyo inaonyesha Chadema hawana imani na tume iliyopo, je CCM watakuwa tayari kukubali kampeni yao hiyo? CCM wako kimya mpaka sasa, ila kuna msemo usemao "ukimuona kobe ameinama ujue anatunga sheria".
Chadema kupitia kampeni yao hiyo watahamasisha wananchi kutoshiriki uchaguzi mkuu endapo hakutokuwa na mabadiliko katika tume ya uchaguzi mkuu. Nawaza tu endapo wananchi wakaunga mkono kampeni hii ni nini kitatokea Tanzania? Vipi kuhusu Chadema plan B na C katika kampeni yao ni ipi endapo wananchi wasipo unga mkono hiyo kampeni.
Wananchi walio wengi wanapenda sana mabadiliko yatokee changamoto ipo hapo kwenye kufanya hayo mabadiliko. Chadema wamewaza kitu kikubwa sana, kuliko zile kampeni za kuandamana ambazo wamekuwa wakifanya bila kuzaa matunda sasa wamekuja na idea kubwa. Hii kampeni haina cha kuandamana, kama kutakuwa hakuna mabadiliko yoyote wananchi watatakiwa kuto kwenda katika vituo vya kupigia kura.
Hivi ikatokea wananchi wakagoma kweli kwenda kupiga kura kipi kitatokea, karibuni katika mdahalo.