Nini maana na dalili za ugonjwa wa pangusa?

Nini maana na dalili za ugonjwa wa pangusa?

mbogyo

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2012
Posts
231
Reaction score
100
Ni muda mrefu toka niwahi kusikia habari za ugonjwa huu lakini huwa najiuliza maana au dokezo la ugonjwa huu na ni nini dalili zake na je ipo tiba? Naombeni msaada wenu wakuu na ahsanteni.
 
CHANCROID
Ni ugonjwa wa ngono unaoshambulia sehemu za siri kwa kuwa na vidonda na uvimbe vinavyoambatana na maumivu makali.

Chancroid ambao kwa kiswahili unaitwa PANGUSA, sio mashuhuri kama magonjwa mengine ya ngono, lakini ni katika magonjwa hatari.

SABABU NA KUENEA KWA UGONJWA HUU

Chancroid inasababishwa na vimelea viitwavyo Haemophilus ducreyi.

Bakteria hawa huingia katika ngozi za sehemu za siri wakati wa kujamiana na mtu mwenye vimelea hii.

DALILI
Mara nyingi bakteria hawa wakiingia ukeni kuna hakuna dalili zinazojitokeza,tofauti kwa
wanaume ambapo dalili zinajitokeza mapema. Baadhi ya dalili ni zifuatazo:

1. Kuwa na kidonda katika uume siku ya 3 au ya 5 baada ya tendo la ndoa. Na kinaendelea kukua na kujitokeza vingine.
2. Kidonda kinakuwa na maumivu makali, na kutoa damu kikiguswa.
3. Kwa wanaume anakuwa na maambukizi katika njia ya mkojo wakati wanawake wanatokwa na uchafu ukeni.
4. Kuwa na mitoki.
5. Kutokwa na usaha katika vidonda.
 
Inawezekana kuupata ugonjwa huu kwa kuvaliana nguo za ndani especially chupi????
 
Back
Top Bottom