Nini maana ya "askari kanzu"?

Nellyonjolo1

Senior Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
120
Reaction score
39
Kiukweli kabisa nimeamini kuwa kila mtu anaweza akawa mwalimu kwa mwenzake na mtu akawa mjinga wa jambo fulani lakini akasita kuuliza..

Kutokana na kwamba kuuliza si ujinga, ujinga ni kuto kujua jambo, Nachukua nafasi hii KUKATAA UJINGA kuuliza jambo ambalo siku nyingi linanitatiza.

:: Nimekua nikilitumia sana na wengine kulitumia neno ASKARI KANZU, Je! ni neno sahihi na lina maana gani? kwanini limetumika neno kanzu? Je, kanzu ina usiri gani katika mavazi ::

Karibuni walimu!! kama kuna mwenye swali la kumuondolea ujinga nae anakaribishwa..
 
asante hata mimi utanisaidia kufuta ujinga kwa hili, tuone wajuvi wakishusha nondo
 

Askari kanzu ni askari alievaa nguo za kiraia akiwepo kazini. Neno kanzu limetumika kwa sababu (wakati wa ukoloni) wenyeji au raia sehemu za pwani huvaa kanzu. Kwa sasa neno kanzu linatumika kama metaphor ya nguo za kiraia.
 

Unaweza tumia hesabu kujifunzia kiswahili. Sijui unanipata?

ASKARI+KANZU = ASKARI-GWANDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…