Nini maana ya b/s kama wanavyoandika ukipima malaria?

Jeff

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2009
Posts
1,293
Reaction score
200
Wadau nina maswali kadhaa naomba mnisaidie
1. ukienda kupima malaria madaktari mnaandika B/S nini maana yake?
2. Kwa nini watoto walioshikana wakati wa kuzaliwa yaani siamen twins hawaezi kula chakula cha aina moja kwa wakati mmoja?
3. Kwa nini mimba ikifika miezi minane na ikitokea mama mja mzito amejifungua mtoto hawezi kuwa mzima ni lazima atakufa, na je ni miezi minane kamili? inakuaje kwa mimba yenye miezi 8 na siku kadhaa mfano na siku 2 au 3 au zaidi?
natanguliza shukrani zangu
 
  1. B/S kirefu chake ni Blood Slide. Hii inweza kuwa thin film au thick film.
  2. Sijui kama unacho kisema hapa ni kweli. Siamies twins ina tegemea ni sehemu gani imeungana. Waweza kuwa mwili mmoja na vichwa viwili, Kichwa kimoja na miili miwili, Wameungana kifuwa na tumbo na nk.
  3. Watoto wakizaliwa pre mature mara zote wanakuwa hawana ukomavu wa mapafu, maini na figo. Lakini hata kama ni miezi 8 akipata care stahili anaweza kuishi bila ya matatizo.
 

Kweli mkuu,

Bado kuna imani za kutisha kwenye medical practices...

Kuna watu wengi wanaamini bundi akilia karibu na nyumba lazima mtu atakufa au degedege haitibiwa hospitali!!

Sijui kama kuna sayansi yoyote inayoweza kueleza kwa nini mtoto njiti wa miaka 8 asiweze kuishi kama facilities za kutosha zipo... Hii ndiyo kwanza naisikia leo!!

Babu DC!!
 
B/s si blood slide bali ni Blood Smear nikwaajili ya kuandaa kupima parasite(vimelea) vya malaria,au leishmania au borrelia pia tryponasomes wanaosababisha sleeping sickness
 
B/s si blood slide bali ni Blood Smear nikwaajili ya kuandaa kupima parasite(vimelea) vya malaria,au leishmania au borrelia pia tryponasomes wanaosababisha sleeping sickness

Asante mkuu Davies,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…