naomba nichangie kama ifuatavyo, tukitaka kupata tafsiri ya neno hili tunaweza kuangalia katika tafsiri za aina nne
1. tafsiri ya neno kwa neno, civic united front ( uraia umoja mbele)
2. tafsiri sisisi, civic united front ( uraia ulioungana mbele)
3, tafsiri ya kisemantiki au maana ( umoja wa uraia mbele )
4, tafsiri ya mawasiliano ni uwakilishi wa umoja wa kiraia. tafsiri ya aina hii (ya kimawasiliano) ndio mara nyingi hutumika katika kutoa tafsiri kutoka katika lugha chanzi au matini chanzi na kwenda katika lugha lengwa au matini lengwa.