Nini maana ya haya maneno katika uchumi

1. Amana ni fedha yako iliyo katika Taasisi za kifedha ambayo unaweza ichukua muda wowote pasipo masharti.

Kwa kifupi kama umedeposi amount kwenye account yako bank kwa ajili ya kuitumia muda wowote hiyo ndio amana
 
3. Sio dhahabu tuu, kuna vito vingine vya thamani vinaweza kutunza thamani ya fedha.
Kama Ardhi inaweza kutunza thamani ya fedha hata madini yanaweza.

Mf. Ukinunua dhahabu ya Tsh. Mil. 10 kisha ukaitunza kwa miaka miwili bila shaka baada ya muda huo lazima itakuwa imepanda bei unaweza kuta imeongezeka mil. 2

So kuliko kutunza fedha ambazo mara nyingi uimara wa sarafu hutegemea sarafu nyingine zenye nguvu duniani. Hivyo ni bora kutunza vitu vya thamani kuliko kutunza fedha
 
Hati fungani hizi ni fedha ambazo mara nyingi Serikali hukopa kwenye soko la fedha la ndani la nchi na kisha fedha hizo Serikali hutumia kutekeleza miradi mbalimbali na kisha baada ya muda fulani Serikali hurudisha fedha hizo kwa wenye nazo na kuwapa faida juu yake.
 
Hati fungani ni namna yoyote ya wananchi kuikopesha kampuni au taasisi. Mathalani, miaka kadhaa iliyopita wananchi waliikopesha NMB, ulisikia wanauza zile hati fungani.

Fedha ambazo serikali inachukua kutoka kwa wananchi ili kutekeleza miradi mbalimbali ni kupitia uuzaji wa amana za serikali.
 
Asante sana kaka Hazchem plate,, umenidadavulia vzr sana na nimekuelewa
 
Ningependa kujifunza maana ya haya maneno katika uchumi;

1. Amana na hati fungani

2. Cryptocurrency

3. Pia, ni jinsi gani dhahabu inakuza/tunza thamani ya fedha
Na je, kuna kimoja wapo hapo kinamaana sawa na "hisa"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…