Nini maana ya "Kaa chonjo"

Nini maana ya "Kaa chonjo"

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
7,553
Reaction score
3,081
Jamani naomba kujua maana ya "Kaa chonjo" maana sielewi kwa sababu linatumika sehemu ambapo sitegemei.
 
Jamani naomba kujua maana ya "Kaa chonjo" maana sielewi kwa sababu linatumika sehemu ambapo sitegemei.
kwa nielewavyo mimi maana yake chukua tahadhari (funguka) kwa kuwa jambo lolote jema au baya laweza kukutokea wakati wowote. mfano mwindaji porini lazima akae chonjo kusubiria mawindo yake yanaweza kupatikana ghafla au vilevile na yeye badala ya kupata mawindo akifikwa na janga kama kuvamiwa na wanyama wakali.
 
Ahsante Rubi,Mimi nilikuwa naelewa vingine kabisa nikisikia kaa chonjo najua kaa pembeni.
 
Jamani naomba kujua maana ya "Kaa chonjo" maana sielewi kwa sababu linatumika sehemu ambapo sitegemei.

Ahsante Rubi, Mimi nilikuwa naelewa vingine kabisa nikisikia kaa chonjo najua kaa pembeni.

Niliposoma comment yako ya mwanzo nilihisi kuwa huenda unakodhani siko kumbe huko ndiko, ila kukaa pembeni inaweza ikawa ni moja ya mbinu ya kuchukua tahadhari kutegemeana na mazingira ya tahadhari iliyopo. Thanks to Rubi for clear explanation.
 
Kaa chonjo= Chukua tahadhari juu suala fulani.
 
Back
Top Bottom