Nini maana ya kuchakachua??

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
54,762
Reaction score
59,204
Wakuu hili neno kiukweli sijajua maana yake kamili labda inawezekana lina maana kubwa au lina maana nyingi. ningeomba wadau wanaojua maana yake halisi waweze kutuelewesha ,manake kwanza hili neno nimeona linatumika sana katika hiki kipindi cha uchaguzi
 
Ni ile hali ya kupindisha ukweli na kuweka uongo, au kutumia usanii usanii badala ya hali halisi ya kitu husika ,linaweza kutumika katika mazingira mbalimbali tu katika elimu,siasa,dini n.k

 

mchakacho = kuchakachua, mchakato = kuchakatua
kwa maoni yangu neno sahihi lingekuwa hilo la pili, yaani kulazimisha mchakato
 
Kuchakachua ni kitendo cha kuchanganya vimiminika viwili tofauti na kufanya kimiminika kimoja, mfano kuchanganya mafuta ya petroli na mafuta ya taa, lakini neno hili sasa limeongezwa matumizi na kuwa linatumika kueleza aina tofauti ya udanganyifu, na kama ulivyoona matumizi ya neno hili sasa yameingia kila mahali kuanzia kwenye kuvuruga matokeo ya uchaguzi hadi kwenye kuelezea watu wadanganifu kwa wapenzi wao1 kwa kifupi sasa ni kama limepoteza ile maana yake ya awali. na inasemekana neno hili asili yake ni uzigua na hasa wazigua wa maeneo ya zaraninge na msata mkoani pwani!
 
Chaka Chua ulikuwa mtindo wa dansi wa bendi ya Urafiki Jazz ya kiwanda cha Friendship Textile Mill pale Ubungo enzi za Mwalimu (vijana wa 70's mpo?). Neno hili hivi sasa limeibuliwa tena na kutumika kivingine kabisaa.
 

Mara nyingi malengo ya kuchakachua ni kudanganya. Mfano, wanaochanganya petrol na mafuta ya taa huwadanganya wateja kuwa hiyo ni petrol pekee,vilevile kuna wanaochanganya maziwa na maji huwadanganya wateja wao kuwa hayo ni maziwa pure.

Kwa kuwa kuchakachua ni kuchanganya vimiminika viwili au zaidi kwa lengo la kudanganya mantiki yake imetumika kuelezea kuchanganya au kubadilisha kitu asili/halisi kwa lengo la kudanganya. Mfano, kuchanganya kura za ukweli na za uongo hivyo kudanganya watu kuwa umeshinda kwa kiasi fulani, kumbe huo sio ushindi wako halisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…