Swali langu ni kama lilivyo hapo juu, nini maana ya kukonyeza.
Kama wewe ni wa kike ukakonyezwa na mwanaume ni nini kitakuja kwenye akili yako yani utatafsiri vipi konyezo hilo na utajisikiaje na kama wewe ni wa kiume, binti akikukunyeza unaweza ukatafsiri vipi na utajisikia vipi?
Kwenye hizi smart phones na gadgets nyinginezo utakuta mtu anakutumia ki-emoji cha 'wink' 😉 ama barabarani, mgahawani ama mahala popote panapokutanisha watu unaweza kuta mtu anakukonyeza.
Je wajua maana yake na wakati gani mtu akitumia konyezo ni halali na wakati gani ni jinai?