Nini maana ya KUTOA RADHI?

Nini maana ya KUTOA RADHI?

mlimbwende

Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
74
Reaction score
26
Waungwana naombeni maana ya neno kutoa radhi. Nini maana yake na nani anatoa radhi na kwa nani? mara nyingi uwa nasikia utapata radhi wewe shauri yako
 
Eeeeh umenikumbusha wimbo wenye maneno haya "Wameshindwa baba na mama wenye kutoa radhi........" wa Twanga
 
kutoa radhi maana yake ni kuchukua(ondoa)radhi toka kwa mtu anayeimiliki hiyo radhi.
 
"Kutoa radhi" ni msemo ambao kwa kweli unabeba maana nzito sana ktk jamii nyingi za Kiafrika. Ktk imani za kijadi, wazazi ni kiungo baina ya nguvu za juu zilizo karibu na Mwenyezi Mungu na waja wake. Nguvu hizo huonekana zaidi pale wazazi wanapotangulia kuungana na wahenga wetu. Wakiwa huko wanaweza zaidi kuingia katika maisha ya wanao ambao bado wapo hapa duniani. Huko waliko wako karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Kwa hakika makabila mengine huwaita wahenga hao "malaika." Ili mzazi aliyetangulia aweze kukusaidia katika maisha yako ya hapa duniani, ni lazima anapoondoka awe amekuwa radhi nawe unayebaki. Akitoa radhi hiyo, basi huna msaada wake. Utahangaika mwenyewe tu. Na pengine anaweza si kuondoa radhi tu, bali pia akakuachia laana. Jambo hili ni baya zaidi. Mtazamo huu wa maisha husisitizwa sana kwa watoto kwa masimulizi ya watu mbalimbali na walivyokosa radhi na matokeo mabaya katika maisha yao. Mifano hai kama hiyo ina nguvu sana katika maisha yetu ya awali.
"Kumwaga radhi" ilianza kama namna moja ya kupindisha dhana hiyo kwa kujifurahisha na kuchekesha wasemaji wa Kiswahili. Na ilianza kwa namna ya kuelezea jambo ambalo mtu akilifanya ni aibu au kashfa fulani. Ni kana kwamba anafanya mambo ambayo yumkini yanawaudhi wahenga. Maana yake kwa sasa ni tofauti kabisa.
 
...ni kumlaani/kumtakia mabaya binadamu mwenzio kwa njia ya maneno au matendo (unavua c*h&&&&u@pi) kutokana na jambo baya alilolitenda machoni pa mtendwaji...watoa radhi wengi huwa ni wazazi/babu/bibi
 
Note : Radhi, Ridhi, Ridhia, Ridhiko, Ridhiana, Kumradhi, na yafananayo na hayo!
Hutokea pale maneno hayo yanapokua kinyume chake!
Aidha radhi si lazima itolewe na mzazi, ipo radhi ya mke kwa mumewe na ya mume kwa mkewe.
 
Back
Top Bottom